JB RASMI ATANGAZA KUSTAAFU KUIGIZA | Tarimo Blog

  


Mkongwe kwenye Tasnia ya Filamu nchini Jacob Steven maarufu kama JB akizungumza na waandishi Wahabari wakati wa uzinduzi wa Tamthilia yake ya Mwisho kuigiza iliyobeba jina la  "Mwanamuziki" iliyoshirikisha Wasanii mbalimbali wa Muziki na WA Filamu iliyozinduliwa katika ukumbi wa Mlimani city jijini Dar es salaam.
Wasanii mbalimbali waliohudhuria Uzinduzi wa Tamthilia ya "Mwanamuziki" katika ukumbi wa Mlimani city jijini Dar es salaam Miongoni mwa ni Monalisa,Matovolwa na wengine pichani.


 Na.Khadija Seif, Michuzi TV

MKONGWE katika Tasnia ya Filamu nchini Jacob Steven maarufu kama JB atupa kete yake ya Mwisho kwenye Tamthilia ya Mwanamuziki kabla ya kustaafu kwake.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tamthilia yake mpya "Mwanamuziki" ambayo imesheheni Wasanii mbalimbali akiwemo patcho Mwamba,Gigy Money,welu Sengo na wengine wengi hususani Wasanii wa Muziki nchini amesema anajivunia kuwa Mkongwe katika Tasnia ya Filamu kwani ameweza kutimiza ndoto za vijana wengi ambao walitamani kufika mbali.

"Katika mikono yangu na kipindi chote ambacho nilikua kwenye tasnia nimweza kuinua vijana wengi hivyo nimeacha alama kwenye kiwanda cha Sanaa ya Filamu na nastaafu nikiwa na Imani kubwa kuwa wao watakuja kuwa alama nzuri Kwa vizazi vijavyo."

Hata hivyo JB ametolea ufafanuzi katika kipindi ambacho atakua nje ya Filamu na namna atashiriki katika Kazi za Sanaa.

"Nina kofia nyingi ikiwemo kucheza Filamu,kuandaa hivyo wakati naenda kustaafu nitahusika zaidi katika kofia ya kuandaa Kazi za Sanaa  na sio kuigiza."

Pia amempongeza waandaji na wanaoendelea kutoa Mchango wao katika Sanaa ya Filamu kwani ndio sababu ya kuona Kazi zao zinaendelea kuthaminiwa.

"Tuzo za Filamu 2021 zimeweza kuonyesha Kwa namnahivyo Serikali inatambua Mchango wa Sanaa ya Filamu na pili Kwa jinsi gani nazalisha vijana wachapakazi kwani waliweza kuonekana Kwa mara ya kwanza kwenye Tamthilia yangu ya "Single Mama" hivyo kupitia Tuzo hizo zitaendelea kuwaibua wengi pamoja na Wasanii hao kuongeza Kasi na uwezo wao na nitaendelea kushirikisha Wasanii chipukizi na ndio maana kwenye Tamthilia hii mpya ya "Mwanamuziki" wapo Wasanii chipukizi wengi ambao tumewapa nafasi."


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2