Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
Chama Cha Mapinduzi (CCM ),Mkoani Pwani kimesema ,kitendo cha ujasiri alichokifanya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Job Ndugai ,kukiri mapungufu baada ya taharuki ya kauli yake kuhusu mikopo wa Serikali si kujidharirisha bali ni kujiimaisha kisiasa kwa vitendo.
Akizungumza na waandishi wa habari , ofisini kwake,Mjini Kibaha Mwenyekiti wa CCM Mkoani Pwani , Ramadhani Maneno alieleza, kitendo cha Spika Ndugai kutoka hadharani kumuomba Radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na Watanzania kijumla kutokana na kauli hiyo tata ni uungwana .
"Kutokana na taharuki hiyo aliyoitoa Ndugai ,takriban wiki moja kwa nchi na watanzania nachukua fursa hii kumpongeza kwa kuonyesha ujasiri kwa kumuomba Radhi Rais Samia Suluhu Hassan na Watanzania kijumla."aliongeza Maneno.
Alimshukuru kwa kuwa jasiri kwani kukiri mapungufu si kujidharirisha ni kujiimaisha.
Maneno alisema kwamba, ombi lake kwa WanaCCM waendelee kuamini kauli ya Spika na kuwa mstari wa mbele kumuunga mkono Rais na maendeleo ya nchi.
January 3 mwaka huu ,Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai alimuomba radhi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan pamoja na Watanzania wote baada ya kuhisiwa kuzungumza maneno ya kuvunja Moyo kuhusu Mikopo wa Serikali.
Spika Ndugai alieleza, hakukuwa na lolote la kurudisha nyuma juhudi za Serikali wala hakuwa na nia ya kukashifu, kudharau juhudi hizo za Serikali ya Tanzania katika kutimiza azma yake ya Maendeleo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment