WAZIRI ASHATU AHIMIZA UPANDAJI MITI | Tarimo Blog


MBUNGE wa Jimbo la Kondoa na Waziri wa Habari,Mawasiliano, na Teknolojia ya habari Habari Mh. Dkt. Ashatu Kijaji, ameanza mwaka kwakuzindua kampeni ya upandaji miti kwenye Jimbo la Kondoa ikiwa ni mkakati wa Kitaifa la kuifanya nchi kuwa ya Kijani.

Tukio hilo limefanyika Mwishoni mwa wiki katika Kata ya Hondomairo kwenye shule ya Sekondari Hondomairo na shule ya msingi shikizi ya Misrey.

Katika zoezi hilo Mh.Dkt. Ashatu aliambatana na Viongozi Mbalimbali wa Chama cha mapinduzi na Serikali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Dkt Hamisi Mkanachi Afisa tawala Wilaya (DAS), Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Kondoa DC, OCD na Kaimu Afisa elimu msingi.

Viongozi wengine walioshiriki zoezi hilo ni wa Chama Cha Mapinduzi CCM (W) ,wataalam toka idara mbalimbali Wilaya ya Kondoa ambazo ni TANESCO, TFS, TARURA pia viongozi mbalimbali walishiriki akiwemo

Aidha katika Mh. Dkt. Ashatu aliongoza zoezi hilo kwa kupanda miche zaidi ya 2,500 kuzunguka shule hizo.

Akizungumza na wananchi wa maeneo hayo mara baada ya kufanisha kupanda miti hiyo Ashatu alisema, suala la utunzaji wa mazingira ni jukumu la kila mwananchi, hivyo agenda ya upandaji miti iwe ni endelevu "tunatamani kuiona Kondoa yetu ya Kijani ndio maana tumesema zoezi letu tulianze siku ya kwanza ya Mwaka 2022 tuanzie hapa Misrey ili tuendelee kwa pamoja kuifanya Misrey ya Kijani, Kondoa ya Kijani na Taifa letu la Kijani. Mazingira yetu ni muhimu sana, miti yetu ni Muhimu sana ndio maana tunaona Leo tunapata mvua za kusuasua sababu ya kuharibu mazingira yetu" alisema Dkt. Kijaji.

Alisema kuwa anatamani kuona Kondoa ya Kijani na Dodoma ya Kijani na himaye nchi kwa ya Kijani kwa kila mmoja kuwajibika kupanda miti katika eneo lake na kuitunza hali ambayo itasaidia kupambana na na mabadiliko ya Tabia Nchi

Sanjari na hilo Pia amesisitiza suala la wazazi kuwapeleka watoto shule kwani hakuna tena kikwazo kwakuwa sasa miundombinu ya shule hiyo shikizi imekamilika vizuri ambapo jumla ya vyumba vya madarasa 10 na kisima cha maji vipo tayari kwa matumizi na ameahidi kutoa Shilingi Milioni tatu kutoka kwenye mfuko wa Jimbo kukamilisha ujenzi wa nyumba ya mwalimu ili shule hiyo ipate usajili hivi mapema.

Nao Wananchi wa Misrey pia wametumia nafasi hiyo kueleza kero mbalimbali zinazowakabili ambazo zilitolewa ufafanuzi na wataalamu mbalimbali waliokuwepo kwenye mkutano huo.

Akifanya majumuisho ya mkutano huo, Mh.Dkt. Ashatu amewasihi wananchi kuongeza jitihada za kujiletea maendeleo katika mwaka huu kwa kutumia vizuri fursa zinazotolewa na serikali makini inayoongozwa na Mhe. Samia Suluhu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ikiwemo kujikita kwenye kilimo cha alizeti kwa kuzingatia Dodoma ni moja ya mikoa mitatu iliyoteuliwa na Mh. Rais kuzakisha alizeti kama zao la kimkakati.

Nao wananchi wa Misrey kwa furaha kubwa wamemshukuru Mh.Mbunge kwa ziara yake na juhudi kubwa za kuikomboa Misrey na Kondoa kwa ujumla kwa kumpatia zawadi ya mbuzi wawili kama sehemu ya kumshukuru.
MBUNGE wa Jimbo la Kondoa na Waziri wa Habari,Mawasiliano, na Teknolojia ya habari Habari  Mh. Dkt. Ashatu Kijaji Akipanda mti kama ishara ya kuzindua zoezi hilo katika jimbo la Kondoa



MBUNGE wa Jimbo la Kondoa na Waziri wa Habari,Mawasiliano, na Teknolojia ya habari Habari  Mh. Dkt. Ashatu Kijaji akipokea zawadi ya Mbuzi 

MBUNGE wa Jimbo la Kondoa na Waziri wa Habari,Mawasiliano, na Teknolojia ya habari Habari  Mh. Dkt. Ashatu Kijaji akizungumza na wananchi

Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Dkt Hamisi Mkanachi akishiriki zoezi la upanda miti Jimbo la Kondoa




Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2