KONGAMANO LA FURSA ZA UWEKEZAJI NA BIASHARA LAFANA | Tarimo Blog

 


Taasisi ya Tafiti za Kiuchumi na Kijamii (ESRF) iliandaa Kongamano la Fursa za Uwekezaji na Biashara lililofanyika katika ofisi za Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam ikiwa na lengo la kuwakutanisha wadau mbalimbali katika sekta za kilimo, ufugaji, teknolojia, , upatikanaji wa mitaji na masoko.

Akizunguma wakati wa kufungua Kongamano hilo Mkurugenzi Mtendaji wa (ESRF), Dkt. Tausi Kida alisema wataalam mbalimbali watawasilisha mada mbalimbali katika fursa ambazo zimefanyiwa tafiti za kina na Taasisi hiyo ambapo mada hizo zimeganyika katika maeneo makuu nne ambazo ni: Fursa zilizopo katika sekta mbalimbali katika mikoa hapa nchini, , Fursa katika Teknolojia, Fursa ya upatikanaji wa masoko pamoja na namna ya kupata mtaji.

Afafanua kuwa katika Kongamano hili, fursa zitakazozungumziwa zaidi itakuwa kwa upande wa Kilimo ambapo Kilimo Biashara ndio itazungumziwa kwa upana zaidi na wataalamu wetu (Kilimo cha mbogamboga bila kutumia udongo “Hydroponic vegetable”, Kilimo cha chakula cha mifugo bila kutumia udongo”Hydroponic fodder” Ukulima katika shamba kitalu “Green House’, ufugaji wa samaki katika vizimba (cage) katika mabwawa (ponds), katika matanki (RAS) “na pia kutakuwa na ushuhuda wa wale ambao wanaofanya Kilimo Biashara.

Kwa upande wa upatikanaji wa mitaji, Dkt. Kida alisema kuwa wafanyabiashara wengi pamoja na wakulima wanapata changamoto kwenye upatikanaji wa mitaji ambapo wengi hawajui namna ya kuweza kupata mitaji au uelewa wa namna ya kupata mitaji, hivyo basi tutakuwa na wataalamu kutoka mabenki na huduma nyingine za utoaji wa mitaji ya kuleta maendeleo kwa watu na taifa kwa ujumla.

Aliongeza kuwa kukua kwa sekta ya teknolojia duniani, sekta zote za maendeleo zinahitaji matumizi ya teknolojia ili kufanya shughuli zake kwa uharaka, uhakika na ufanisi mkubwa ambao utaleta tija. Kwa kuliona hilo tumewaalika wataalamu ambao leo hii watatoa mada juu ya matumizi wa teknolojia na jinsi teknolojia inavyotumika katika kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla. Lakini pia tutakuwa na mashuhuda wa matumizi wa teknolojia ambao wanafanya vyema katika shughuli zao.

Alisistiza kuwa Fursa zilizopo hapa nchini ni nyingi sana kwani kila mkoa wa Tanzania una fusra zake na hasa kwenye kilimo, ufugaji pamoja na madini hivyo amewaasa vijana kuchangamkia fursa hizo ili kujikwamua kiuchumi.

Akitoa salamu kwa niaba ya Wizara ya Kilimo, Kaimu Mkurugenzi wa Kilimo upande wa Sera na Mipango ndugu Gungu Mibavu, alisema serikali iko bega kwa began a wadau wote wa Kilimo kwa kuhimarisha shughuli za ugani pamoja na kutoa kodi na tozo ambazo zimekuwa kero kwa wadau wa Kilimo.

Alisistiza kuwa Fursa zilizopo hapa nchini ni nyingi sana kwani kila mkoa wa Tanzania una fusra zake na hasa kwenye kilimo, ufugaji pamoja na madini hivyo amewaasa vijana kuchangamkia fursa hizo ili kujikwamua kiuchumi.

Wadau walioshiriki kwenye kongamano hilo ni Wizara ya Kilimo. Wizara ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara, Kituo cha Uwekezaji Tanzania(TIC), Jeshi la Kujenga taifa(JKT), Aquaculture Association of Tanzania, Big Fish, Agriculture Media Ltd, Green Fish Investment, Nyanzobe Ltd, IMADS, Tanganyika Apicultural Ltd, Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo(SIDO), Multics Company. Ramani, Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania(TANTRADE), SSC Capital, CRDB, TADB, SELF pamoja na PASS.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF), Dk. Tausi Kida akizungunza kuhusu namna walivyojipanga kuendelea kufanya tafiti pamoja na kutoa elimu ili kuwainua wananchi mbalimbali kwenye sekta ya kilimo, Biashara pamoja na teknolojia wakati wa kufungua Kongamano Kongamano la fursa za Uwekezaji na Biashara lililofanyika katika ofisi za taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Dkt. Daniel Ngowi kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) akizungumzia fursa zilizopo pamoja na upatikanaji wake katika mikoa mbalimbali ya hapa nchini wakati wa Kongamano la fursa za Uwekezaji na Biashara lililofanyika katika ofisi za taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Msaidizi wa Sera, na Mipango kutoka Wizara ya Kilimo, Gungu Mibavu akizungumza kuhsu namna serikali ilivyojipanga kuwasaidia wakulima pamoja na wafugaji ikiwa mi pamoja na kuwaondolea vikwazo ili kuweza kuongeza pato la taifa wakati wa Kongamano la fursa za Uwekezaji na Biashara lililofanyika katika ofisi za taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam
Meja Kelvin Ngondo Kutoka Jeshi la KujengaTaifa (JKT) akizungumza kuhusu Kilimo Biaishara hasa kwenye Ufugaji wa samaki kisasa kwa kutumia Vizimba, Matanki na mabwawa wakati wa Kongamano la fursa za Uwekezaji na Biashara lililofanyika katika ofisi za taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam
Mr. Raphael Majivu Kutoka Agriculture Media Ltd akitoa mada kuhusu kilimo cha kisasa cha chakula cha mifugo bila kutumia udongo (Hydroponic Fodder & Azolla) wakati wa Kongamano la fursa za Uwekezaji na Biashara lililofanyika katika ofisi za taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam
Afisa Mipango na Uwekezaji kutoka Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo(SIDO), Johari Masengi akitoa mada kuhusu fursa zilizopo katika Shirika hilo ili kukuza Biashara na Uwekezaji kwa wafanyabishara wadogo wakati wa Kongamano la fursa za Uwekezaji na Biashara lililofanyika katika ofisi za taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Philemon Kiemi Kutoka Tanganyika Apicultural Ltd akitoa mada kuhusu fursa zilizipo katika Ufugaji wa kisasa wa nyuki pamoja na bidhaa mbalimbali za nyuki wakati wa Kongamano la fursa za Uwekezaji na Biashara lililofanyika katika ofisi za taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Ian Usiri Kutoka ya Ramani akitoa mada kuhusu fursa za Kibiashara na Uwekezaji kidigitali zinavyoweza kuongeza kipato pamoja na namna unavyoweza kufanya kazi za kimtandao wakati wa Kongamano la fursa za Uwekezaji na Biashara lililofanyika katika ofisi za taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wadau mbalimbali wa Kilimo na Ufugaji waki fuatilia mada mbalimbali kwenye Kongamano la fursa za Uwekezaji na Biashara lililoandaliwa na Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF) lililofanyiaka katika ofisi za Taasisi hiyo Dar es Salaam.



Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2