LUKUVI NA KABUDI NIMEWAVUTA WAJE KWANGU, TUSAIDIANE KUSIMAMIA WENGINE- RAIS SAMIA | Tarimo Blog

*Azungumzia Lukuvi kuhusishwa kugombea U-Spika

Na Said Mwishehe, Michuzi TV
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amesema kuwa aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi pamoja na aliyekuwa Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi atakuwa nao kwenye ofisi yake ili kuhakikisha wanashirikiana wote kuwasimamia viongozi wengine.

Akizungumza leo Januari 10,2022 wakati wa shughuli ya kuapisha viongozi mbalimbali wakiwemo Mawaziri na Manaibu Mawaziri , Makatibu Wakuu pamoja na Makatibu Wakuu iliyofanyika Ikulu ya Chamwino Mjini Dodoma, Rais Samia amesema Lukuvi na Profesa Kabudi amevuta ofisini kwake na watapangiwa majukumu mengine.

Amesema Profesa Kabudi na Lukuvi wao amewaondoa katika Baraza la Mawaziri kwasababu anataka awe nao katika ofisi yake kwa ajili ya kumsaidia katika kusimamia wengine walioko kwenye nafasi mbalimbali ambazo wameteuliwa na kuapishwa kuzitumikia.

"Hawamo katika Baraza la Mawaziri kwasababu Lukuvi na Kabudi nimewavuta waje kwangu, ukiwangalia mri wao ni kama wangu, na wale ambao nimewateua kule wengi ni vijana, hivyo tutashirikiana kusimamia wale ambao tumewapa nafasi.Waziri Kabudi amefanya kazi kubwa na nzuri ya kusimamia mazungumzo ya mikataba kati ya Serikali na Mashirika ya umma.

"Hivyo huku kwangu pamoja na mambo mengine Prof.Kabudi atakuwa ndio Baba mikataba, Baba majadiliano.Lukuvi naye atakuwa pamoja na mimi, tunakwenda kuwasimamia ninyi(niliowateua).Lukuvi hatagombania Uspika, Lukuvi ametumikia Taifa hili kwa uadilifu mkubwa, hivyo tusimchafue.

"Nitakuwa naye katika ofisi yangu katika kuwasimimia wengine,ukiangalia umri wa Lukuvi na Kabudi wao wamebakisha mwaka mmoja , miaka miwili wastaafu, hivyo nitastaafu nao."amesema Rais Samia

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2