Katibu wa Mtandao wa Vijana wa Manispaa ya Temeke, pia Mratibu wa Mradi wa School 2030, Yusufu kutegwa akioa mafunzo kwa vijana wa Manispaa ya Temenke jijini Dar es Salaam.
Mtoa maunzo akipitia kwa baadhi ya vijana wakati wakitoa mafunzo katika darasa la utekelezaji wa Maradi wa School 2030 unaendeshwa katika manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya vijana wa Manispaa ya Temeka wakiwa katika Darasa la Ujasiliamali na kujitambua ambalo huanyika kila wiki Ijumaa hadi jumapili katika shule ya Msingi Azimio iliyopo Manispaa hiyo.
MANISPAA ya Temeke kupitia Mradi wa School 2030 wapo katika majaribio ya utekelezaji wa Mradi huo unaolenga kutatua changamoto za Vijana walio nje ya mumo rasmi wa elimu hapa nchini na kuwatautia utaratibu wa kujifunza ili kutatua changamoto wanazokumbana nazo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Katibu wa Mtandao wa Vijana wa Manispaa ya Temeke, pia Mratibu wa Mradi wa School 2030, Yusufu kutegwa amesema kuwa lengo la kutekeleza Mradi huo ni kutokana na changamoto ambazo Vijana wanakumbana nazo.
Amesema kuwa Mradi wa School 2030 unachukua Vijana wasio katika mfumo wa elimu kuanzia miaka 14 hadi miaka 24 wa Manispaa ya Temeke.
Amesema Mradi huo utawaelekeza Vijana kutambua changamoto wanazozipitia pamoja na kujua namna ya kuzitatua.
"Vijana wanakumbana na changamoto mbalimbali katika jamii na kiuchumi lakini kupitia mafunzo yanayotolewa na mradi wa School 2030 unaweza kuleta suluhisho la kukabiliana na changamoto za kijamii na kiuchumi." Amesema Kutegwa
Amesema kuwa mafunzo yanayotolewa ni ya stadi za maisha na stadi za ujasiliamali zitakazowawezesha kujitambua, kufanya maamuzi sahihi, kujua namna ya kuhimili misongo na mihemko, kujua namna ya kuwasiliana na makundi rika, kuwasiliana na watu wazima na kufanya mawasiliano yenye tija Kwa jamii.
Amesema kuwa watawafundisha Vijana namna gani ya kupata kipato kupitia miradi ambayo watakwenda kuanzisha mara baada ya kupata mafunzo.
Amesema Mradi huo upo katika majaribio ya Vijana 40 wa kata ya Azimio katika Manispaa ya Temeke, amesema Vijana hao wakifanya vizuri wataangalia namna ya kuongeza kata za Manispaa hiyo.
Amesema Manispaa ya Temeke inakata 23 hivyo baada ya kufanikiwa Mradi huo watachukua Vijana katika kata zote za Manispaa hiyo.
Amesema tatizo la kukosa ajira ni kubwa katika Manispaa hiyo hivyo Vijana walio nje ya mfumo wa shule hawapati taarifa sahihi za fursa za ajira zilizopo katika Manispaa hiyo.
Kwa upande wa wanufaika wa Mradi huo, Eliabu Ejege amesema kuwa mafunzo hayo yatamsaidia kufikia malengo yake kwani wanafundishwa mbinu mbalimbali za kufanya biashara pamoja na kujitambua.
Amesema kuwa mwisho wa Mradi huo wataunda vikundi vya Vijana watano watano kila kikundi kitatakiwa kubuni wazo la biashara na watawezeshwa Kwa kupewa mikopo itakayowasaidia kuendesha biashara zao.
Kwa Upande wa Mwaija Othman amesema mafunzo ya miezi mitano yanayotolewa Kwa Vijana kwaajili ya kujitambua na kuwa na mawazo chanya juu ya changamoto zinazojitokeza katika jamii.
Amesema mpaka kumalizika Kwa mafunzo hayo atakuwa tofauti na alivyokuwa mwanzo kwani anafikra huru na anahamasa kubwa kwaajili ya kuwahamasisha Vijana wengine ili waweze kujikwamua katika mawazo hasi walinayo.
Kwa Upande wa Lukia Sijaona amewashukuru waendeshaji wa mafunzo hayo kwani mafunzo hayo wataweza kuwa na ujasiri wa kuanzisha biashara mbalimbali Kwa kutumia mawazo Yao wenyewe.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment