WANAFUNZI WAKIKE 28914 WALIACHA SHULE KATI YA 2015 HADI 2019, JINSI SERIKLAI ILIVYOWAJIBIKA KWAWAREJESHA SHULENI | Tarimo Blog

*Wanafunzi wa kike 28914 wakatisha masomo ndani ya miaka minne

Na Avila Kakingo, Michuzi TV
TAKWIMU za elimu za mwaka 2020 zinaonesha kuanzia mwaka 2015 hadi 2019 wanafunzi wakike 28914 walikatika masomo kwa sababu ya ujauzito hii ikasabaisha Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupoteza nguvu kazi ya taifa kwa idadi hiyo ndani ya miaka mitano.

Hivyo kwa mwaka mwaka 2015 hadi mwaka 2019 wanafunzi wa kike 4205wa shule ya msingi na shule ya sekondari 24,709 walikatisha masomo huku idadi yao ikitofautiana mwaka hadi mwaka.

Kutokana na tamko la Waziri wa Elimu, sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako lililotolewa Novemba 24, 2021 kuhusu wanafunzi waliokatiza masomo kwa sababu ya kupata ujauzito kurejea shuleni kupitia mfumo ramsi hii itapunguza utegemezi.

Tamko hilo lilifuatiwa na walaka uliosainiwa na Kamishna wa Elimu Dkt. Lyabwene Mtahabwa ukiwa ni waraka elimu No. 2 wa mwaka 2021, sasa kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania (Bara) watoto walioacha shule kutokana na changamoto mbalimbali ikiwemo watoto wakike walioacha shule kwa sababu za kupata ujauzito watarudi shuleni kuendelea na masomo yako kupitia mfumo rasmi wa elimu.

Katika tamko la Hakielimu lililotolewa na Mkurugenzi Mtendaji, Dkt. John Kalage lilieleza, Pamoja na msukumo mkubwa iliyopata serikali kutoka kwa watetezi wa haki elimu na elimu kwa mtoto wa kike serikali sasa imeridhia mtoto wa kike kurudi kurudi shuleni katika mfumo rasmi hata baada ya kujifungua.

Dkt. Kilage ameeleza kuwa hatua na msukumo huo ulikuwa si tu kumyima mtoto wa kike fursa ya kumaliza masomo na kujiendeleza kitaaluma bali ulikuwa ukirudisha nyuma taifa kimaendeleo kwa kukumbatia sehemu kubwa ya kizazi cha kesho kisichoelimika ipasavyo na hivyo kurudisha nyuma kimaendeleo.

Hakielimu wametoa wito kwa serikali kukazia tamko na azma kwa kuihuisha miongozo maalumu inayowezesha mtoto wa kike kurudi shuleni baada ya kujifungua ya mwaka 2009, ambayo iliandaliwa lakini haikutiwa saini kutokana na msimamo wa serikali ilipita juu ya watoto wa kike waliopata ujauzito kurudi shuleni.

Amesema miongozo hiyo ilieleza hatua kwa hatua ya namna ya mtoto wa kike anavyoweza kurudi shuleni baada ya kujifungua pamoja na kutoa waraka No. 2 wa Elimu wa 2021 unatoa maelekezo ya kumruhusu mtoto wa kike kurudi shuleni lakini haujitoshelezi katika vipengele vya hatua gani zichukuliwe ili mtoto huyo arudi shuleni bila kubaguliwa, akijiamini pamoja na kulinda haki za mtoto aliyezaliwa ya kupata malezi ya mama kama kunyonya ba kuhudumiwa.

Hivyo ameshauri selikari kuandaa miongozo na kuanza kutumika mapema ili kutoa fursa kwa mtoto wa kike aliyeacha shule kati ya 2019 hadi 2020 aweze kurudi shule rasmi kuanzia mwaka wa masomo wa 2022.

Ameshauri kuanyiwa marekebisho kwa Sheria ya Elimu ya mwaka 1978, Sera ya elimu ya 2014 na katika mwongozo wa sheria ya Elimu unaruhusu ufukuzwaji na usimamishaji wa masomo wa watoto walioko shuleni, wanaopata ujauzito au kufanya makosa mengine.

Katika kuhakikisha watoto wote wanaendelea kupata fursa ya elimu kama haki yao ya msingi kupitia waraka No. 2, serikali inatoa fursa kwa wanafunzi wanaoacha shule kutokana na kupata ujauzito wakiwa shuleni kurejea katika mfumo rasmi wa elimu.

Ikumbukwe kuwa kabla ya uamuzi huo watoto wakike waliopata ujauzito kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kubakwa, ndoa za utotoni au kurubuniwa walifukuzwa shule moja kwa moja na hawakuruhusiwa tena kujiunga na masomo ya elimu ya msingi na sekondari popote pale nchini.

Akizungumzia kuhusu haki ya mtoto ya kupata elimu, Mratibuwa Mradi wa Ulinzi na usalama kwa watoto kutoka Kituo cha Msaada wa Kisheria kwa Wanawake na Watoto (WILAC), Wakili Abia Richard amesema maamuzi ya serikali kuruhusu watoto waliopata ujauzito wakiwa shuleni la jambo zuri na la kuipongeza serikali.

“Hata sheria zinasema mtoto chini ya miaka 18 ukifanya nae mapenzi umembaka na sasa iwaje mtoto huyo huyo aliyeanyia ukatili wa ubakaji bado aanyiwe ukatili mwingine wa kunyimwa elimu, ukiangalia inakuwa sio haki maana mtoto sio mkosaji katika kubeba mimba bali ni mhanga wa vitendo vya ukatili wa kingono na anahitaji msaada ili atimize ndoto zake.” Amesema Wakili Abia

Amesema kuwa takwimu zinaonesha wanafunzi 1887 walipata ujauzito kwa mwaka jana na wakinyimwa haki ya kupata elimu hivyo Serikali ya awamu ya tano imefanya jambo kubwa katika kumkwamua mtoto wa kike ili aweze kuzifikia fursa mbalimbali zinazojitokeza kwenye sekta ya elimu.

Kwa upande wa Mwanahamis Kasimu (17) ambaye alitakiwa kuwa kidato cha tatu mpaka sasa alisema sababu ya yeye kukatisha masomo ni kupata ujauzito kutokana na ugumu wa maisha pamoja na kuhamahama kwa mama yake mara baada ya baba yake kufariki dunia.

Kwa upande wa Nuru Mahamud amesema kuwa changamoto za maisha na mzazi wake ndio kulikopelekea kuwa na mwanaume ambaye alikuwa anampa mahitaji madogo madogo na ndicho kilichompelekea yeye kupata ujauzito akiwa darasa la saba na mpaka sasa anasema hata ikitokea nafasi kurudi shule hatorudi kwani anaona aibu kusoma na wanafunzi ambao ni wadogo kuliko yeye.

Kwa upande wa Twahiba Shamte amewaasa wanafunzi ambao wanaendelea na masomo kujilinda wasipate Ujauzito wakiwa shuleni huku akiomba wasijiingize katika mambo ya ndoa kwa wao bado wadogo.
Mwandishi wa Michuzi blog katikati, Avila Kakingo akiwa katika picha ya pamoja mahojiano leo Januari 5, 2022 na wanafunzi waliokatisha masomo wakiwa shuleni kwa sababu ya kupata ujauzito kulia ni Nuru Mahmud na kushoto ni Mwanahamis Kasimu

Mwandishi wa Michuzi blog katikati, Avila Kakingo akiwa katika picha ya pamoja mahojiano leo Januari 5, 2022 na wanafunzi waliokatisha masomo wakiwa shuleni kwa sababu ya kupata ujauzito kulia ni Lailat Kasimu na kushoto ni Twahiba Shamte.
Kielelezo kinaonesha jinsi wanaunzi wa kike jinsi walivyoacha masomo kwa sababu ya matatizo mbalimbali ikiwemo kupata ujauzito.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2