Na Mwandishi wetu, Babati
NAIBU Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kumuamini na kumuacha kwenye Baraza la Mawaziri ikiwemo mabadiliko yaliyofanyika juzi.
Gekul ameyasema hayo wakati akizungumza jana kwenye ibada iliyofanyika Mjini Babati Mkoani Manyara katika Kanisa la Afrika Mashariki (K.K.A.M) ambapo amemshukuru Mungu kwa yeye kuendelea kuaminiwa na Rais Samia.
Naibu Waziri huyo ambaye ni mbunge wa jimbo la Babati mjini amesema Kanisani hapo kuwa anamshukuru Mungu kwa Rais Samia kuendelea kumuamini hivyo ameahidi kuendelea kufanya kazi kwa bidii ili kulinda heshima na imani kubwa aliyopewa na Rais.
"Namshukuru Mungu kwa hili kwani Rais Samia ameendelea kuniamini kwa mara ya tatu mfululizo amefanya mabadiliko ya mawaziri na manaibu na mimi kubaki ili nimsaidie kazi," amesema Gekul.
Amewaomba waumini wa kanisa hilo na wananchi kwa ujumla kumuunga mkono Rais Samia na kumpa ushirikiano ili afanikishe maendeleo kupitia miradi mbalimbali ya kimkakati.
Hata hivyo, amewaomba viongozi wa dini kuendelea kutoa mafundisho ya maadili kwa vijana ili kuepuka kuwa na Taifa lisilokuwa na nidhamu.
Amewaomba wananchi ambao hawajapata chanjo ya kupambana na uviko-19 kuchangamkia fursa hiyo ili kuepuka madhara yanayosababishwa na ugonjwa huo.
Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini Mkoani Manyara, akizungumza kwenye Kanisa la Afrika Mashariki (K.K.A.M) Mjini Babati, kwenye ibada ya kumshukuru Mungu kwa yeye kuendelea kuaminiwa na Rais Samia Suluhu Hassan
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment