Na Mwandishi Wetu, Chalinze.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mh. Ridhiwan Kikwete ameendelea na ziara yake maalumu ikiwemo kutatua migogoro ya ardhi, sambamba na kukagua maboma ya majengo ya shule na huduma za afya yanayojengwa kwa fedha za maendeleo.
Mh. Ridhiwan Kikwete emeweza kutembelea Kata ya Lugoba katika Vijiji vya Mindutulieni, Kinzagu na Lugoba ambapo kote huko ameweza kufanya mikutano ya wazi kusikia na kupokea kero na maoni ya wananchi.
Akiwa katika ziara hiyo, Mh. Ridhiwan Kikwete alibainisha kuwa ofisi yake na yeye kama Mbunge watahakikisha wanafika kwa Wananchi mara kwa mara ilikusikiliza na kutatua kero zao zinazowakabiri huku zile zingine akizipokea na kuziwasilisha ngazi za juu ikiwemo Bungeni na Serikalini.
"Hatua zinazochukuliwa kutatua migogoro ya ardhi inayosababisha na watu wasiofuata taratibu ndiyo zinazitaraji kuwa chachu ya kurudisha amani na maendeleo katika miji yetu…”Alibainisha Mh. Ridhiwani Kikwete
Aidha, aliendelea kutoa shukrani kwa Serikali chini ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan kwa kuweza kutoa fedha zilizosaidia na zinazoendelea kusaidia miradi mbalimbali ndani ya Halmashauri na Jimbo hilo la Chalinze ikiwemo Bilioni 1.7 katika ujenzi wa Madarasa, mabweni na huduma za afya ikiwemo ujenzi wa vituo vya Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali.
"Chalinze kazi zinaendelea, Wanachalinze kila kona wanafurahia matunda mema ya Serikali chini ya Rais wetu Mh. Samia Suluhu Hassan." Alimalizia Mh. Ridhiwan Kikwete.
Akiwa katika kijiji cha Mindutulieni alipata wasaha wa kukagua jengo la (boma) la Zahanati ya Mindutulieni.
Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mh. Ridhiwan Kikwete akizungumza katika mkutano wa wazi na Wananchi wa Kijiji cha Mindutulieni, tarehe 7, Januari 2022.Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Mh. Ridhiwan Kikwete akizungumza na Wananchi wakati wa kukagua jengo (boma) la Zahanati ya Mindutulieni wakati wa ziara yake ndani ha Jimbo hilo tarehe 7, Januari,2022.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment