WAHANDISI WANAWAKE WASISITIZWA KUJISAJILI NA BODI YA WAHANDISI | Tarimo Blog

Wahandisi wanawake kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi,(Sekta ya Ujenzi), kitengo maalumu cha ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara, wakiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia (MUST), jijini Mbeya mara baada ya kutoa elimu inayohusiana na masuala ya Ujenzi, ikiwemo Uhandisi, Ubunifu Majengo na Ukadiriaji Majenzi.
Mhandisi kutoka Bodi ya Ubunifu Majengo na Ukadiriaji Majenzi (AQRB), Mhandisi Shangwe kambaga, akizungumza na Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo cha Sayansi na Teknlojia (MUST), mara baada ya kutoa elimu kuhusu masuala mbalimbali ya ubunifu wa majengo wa majengo jijini Mbeya.
Baadhi ya wanafunzi kutoka Chuo cha Sayansi na Teknolojia (MUST), Jijini Mbeya wakimsikiliza Mhandisi Nancy Mduma (hayupo pichani), kuhusu umuhimu wa kujisajili na Bodi ya Wahandisi (ERB) pindi wanapomaliza vyuo.
Mhandisi kutoka Bodi ya Usajili Wahandisi (ERB), Mhandisi Nancy Mduma akifafanua jambo kwa Wanafunzi wa Chuo cha Sayansi na Teknolojia-MUST, (hawapo pichani), Jijini Mbeya.

SERIKALI kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, (Sekta ya Ujenzi), imewataka wanafunzi wote wa kike kutoka vyuo mbalimbali wanaosomea fani zinazohusiana na Ujenzi kuweza kujisajili katika Bodi ya Usajili wa Wahandisi (ERB), ili kuingia katika mfumo maalumu wa kihandisi.

Hayo yameelezwa na Mhandisi Nancy Mduma kutoka Bodi ya Usajili Wahandisi (ERB), wakati akifungua semina elekezi kwa wanafunzi wa kike kutoka chuo cha Sayansi na Teknolojia (MUST), kwenye ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara.

Mhandisi Mduma amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa sana kwa wahandisi wanaomaliza vyuo kujisajili katika bodi hiyo kwani kuna kazi nyingine za kihandisi zinataka mhandisi aliyesajiliwa tu.

“Serikali sasa inalenga kuwawezesha wahandisi wanawake kufikia madaraja ya juu ya uhandisi, na hili kufikia madaraja hayo ni bora kila mhandisi baada ya kumaliza chuo aweze kujisajili na kuingia kwenye mfumo wa Bodi ya Wahandisi,” amesisitiza Mhandisi Nancy

Kwa upande wake Mratibu kutoka Bodi ya Usajili Wakandarasi (CRB), Mhandisi Victoria Haule amesema kuwa kazi kubwa ni kuwahamasisha Wanawake kushiriki katika kazi za Barabara ili kuongeza wigo mkubwa wa maendeleo unaofanywa na wanawake kutoka sehemu mbalimbali.

Aidha, katika mada nyingine zilizotolewa ni pamoja na kuangalia mchakato wa usajili kwa makampuni ya wanawake, kupitia mwongozo wa kuimarisha ushiriki wa wanawake katika kazi za barabara na masuala mtambuka.

Zaidi ya wanachuo 70 wameweza kushiriki katika Uwasilishwaji wa mada mbalimbali zinazohusu kushiriki kazi za barabara.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2