Benki ya Exim imekabidhi gari aina ya Toyota Vanguard kwa taasisi ya Work of Mary (Focolare Movement Tanzania) ya mkoani Iringa iliyoibuka mshindi wa zawadi kubwa ya promosheni ya “Weka Mkwanja tukutoe!” iliyokuwa ikiendeshwa na benki hiyo ikilenga kuhamasisha wateja wake kujiwekea akiba.
Akizungumza kwenye hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika mapema hii leo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa idara ya wateja wadogo na kati Benki ya Exim Bw Andrew Lyimo alisema mshindi huyo ni miongoni mwa wateja wa benki hiyo waliofanya miamala kuanzia kiasi cha Tsh laki tano (500,000) na kuendelea ambapo aliweza kuingia moja kwa moja kwenye droo kubwa ya kujishindia gari aina ya Toyota Vanguard na hivyo kuibuka mshindi wa zawadi hiyo kubwa.
“Mbali na mshindi huyu wa zawadi kubwa, washindi wengine 18 waliweza kujishindia zawadi ya fedha taslimu mil 1 kila mmoja katika droo mbalimbali zilizokuwa zikiendeshwa kwa usimamizi wa Bodi ya Michezo ya kubahatisha katika kipindi chote cha kampeni.’’ Alisema Lyimo huku akiwashukuru wateja kwa muitikio mzuri katika kampeni hiyo.
Alisema sambamba na zawadi hizo kampeni hiyo iliambatana na utoaji wa elimu kwa wateja wa benki hiyo ikilenga kuwahamasisha kujiwekea akiba na faida zake katika kufikia malengo yao kiuchumi.
“Kampeni hii ilikuwa ni moja ya njia ya benki ya Exim katika kukuza utamaduni wa kuweka akiba hapa nchini ili kuongeza tija katika maendeleo ya taifa.’’alibainisha.
Akizungumza kuhusu mafanikio ya kampeni hiyo, Lyimo alisema, katika kipindi cha miezi mitatu ya kampeni hiyo benki hiyo iliweza kuvutia wateja wapya zaidi ya elfu 6 huku ikifikisha malengo yake kuongeza amana na akiba za wateja kwa asilimia 110%.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Muwakilishi wa taasisi ya Work of Mary (Focolare Movement Tanzania) Bi Christina Maria Da Silva aliishukuru Benki ya Exim kwa zawadi hiyo ya gari huku akibainisha siri ya ushindi ni kutumia benki hiyo kujiwekea amana.
“Kwa upande wetu taasisi ya Work of Mary tunayo furaha kubwa kupokea zawadi hii kutoka Benki ya Exim. Zaidi, tumekuwa tukifurahishwa na huduma tunazozipata kutoka benki hii kupitia tawi la Iringa. Tunawahamasisha na wa Tanzania wengine wafungue akaunti katika benki ya Exim kwa ajili ya kupata huduma bora za kibenki ikiwepo huduma kurahisishwa kupitia mifumo ya kidigitali ambapo unaweza fanya mihamala ya kibenki ukiwa ofisini au majumbani kwako kwa njia salama kabisa, alisema.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo Bw Stanley Kafu alimpongeza mshindi huyo pamoja na washindi wengine waliopatikana kupitia kampeni hiyo huku pia akiwasihi wateja wa benki hiyo kuendelea kufurahia huduma za benki hiyo sambamba na kuchangamkia kampeni nyingine kama hizo kupitia benki hiyo.
Mwisho.
Viongozi waandamizi wa Benki ya Exim wakiongozwa na Mkuu wa idara ya wateja wadogo na kati Benki ya Exim Bw Andrew Lyimo (wa tatu kushoto) wakibadhi nyaraka za umiliki wa gari aina ya Toyota Vanguard kwa Muwakilishi wa taasisi ya Work of Mary (Focolare Movement Tanzania) ya Mkoani Iringa, Bi Christina Maria Da Silva (kulia) baada ya taasisi hiyo kuibuka mshindi wa zawadi hiyo kubwa ya promosheni ya “Weka Mkwanja tukutoe!” iliyokuwa ikiendeshwa na benki hiyo ikilenga kuhamasisha wateja wake kujiwekea akiba. Hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Wengine ni pamoja na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo Bw Stanley Kafu, Mkuu wa Idara ya Mtandao wa Wateja wa benki ya Exim Bi. Agnes Kaganda pamoja na wawakilishi wengine wa taasisi ya Work of Mary.
Mkuu wa idara ya wateja wadogo na kati Benki ya Exim Bw Andrew Lyimo (wa tatu kushoto) akibadhi nyaraka za umiliki wa gari aina ya Toyota Vanguard kwa Muwakilishi wa taasisi ya Work of Mary (Focolare Movement Tanzania) ya Mkoani Iringa, Bi Christina Maria Da Silva baada ya taasisi hiyo kuibuka mshindi wa zawadi hiyo kubwa ya promosheni ya “Weka Mkwanja tukutoe!” iliyokuwa ikiendeshwa na benki hiyo ikilenga kuhamasisha wateja wake kujiwekea akiba. Hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika mapema hii leo jijini Dar es Salaam. Wengine ni pamoja na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo Bw Stanley Kafu (wa pili kulia) Mkuu wa Idara ya Mtandao wa Wateja wa benki ya Exim Bi. Agnes Kaganda (wa nne kulia) pamoja na wawakilishi wengine wa taasisi ya Work of Mary.
Akizungumza kwenye hafla hiyo, Muwakilishi wa taasisi ya Work of Mary (Focolare Movement Tanzania) Bi Christina Maria Da Silva (Pichani) aliishukuru Benki ya Exim kwa zawadi hiyo ya gari huku akibainisha siri ya ushindi ni kutumia benki hiyo kujiwekea amana.
Wafanyakazi wa Benki ya Exim wakiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi wa taasisi ya Work of Mary (Focolare Movement Tanzania) ya Mkoani Iringa wakati wa hafla ya makabidhiano ya gari aina ya Toyota Vanguard kutoka Benki ya Exim kwenda kwa taasisi hiyo iliyoibuka mshindi wa zawadi kubwa ya promosheni ya “Weka Mkwanja tukutoe!” iliyokuwa ikiendeshwa na benki hiyo ikilenga kuhamasisha wateja wake kujiwekea akiba. Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Muwakilishi wa taasisi ya Work of Mary (Focolare Movement Tanzania) ya Mkoani Iringa, Bi Christina Maria Da Silva akikagua gari aina ya Toyota Vanguard wakati akikabidhiwa gari hiyo na Benki ya Exim ikiwa ni zawadi kwa taasisi hiyo baada kuibuka mshindi wa zawadi kubwa ya promosheni ya “Weka Mkwanja tukutoe!” iliyokuwa ikiendeshwa na benki hiyo ikilenga kuhamasisha wateja wake kujiwekea akiba. Hafla ya makabidhiano hayo iliyofanyika mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment