HAKUNA NJIA YA MKATO KUUPUNGUZA UNENE, KUACHA KULA UNASABABISHA MADHARA MENGINE MWILINI- DK.GRACE | Tarimo Blog


 Na Said Mwishehe, Michuzi TV

WATANZANIA wameshauriwa kuifanyisha miili yao mazoezi kama sehemu mojawapo ya kukabiliana na kujiepusha na magonjwa yasiyoambikiza huku wakielezwa hakuna njia ya mkato ya kupunguza mwili.

Ushauri huo umetolewa na Dk.Grace Moshi kutoka Idara ya Kinga Kitengo cha Huduma za Lishe Wizara ya Afya alipokuwa akichangia mada iliyokuwa inazungumza umuhimu wa ufanyaji mazoezi na kubadilisha mtindo wa maisha ambao unatajwa kama moja ya sababu ya kuongezeka kwa magonjwa yasiyoambikiza nchini.

Akifafanua zaidi kwa washiriki wa mkutano ulioratatibiwa na Shirikisho la Vyama vya magonjwa yasiyoambikiza Tanzania( TANCDA) kwa lengo kuwasilishwa muhtasari wa Sera juu ya lishe na kushughulisha mwili Dk.Grace Moshi ameeleza ni jinsi gani unatakiwa kupunguza mwili bila kuathiri mfumo wa mwili.

"Ni muhimu kuufanyisha mwili mazoezi na unapoufanyisha mazoezi hakikisha inakwenda sambamba na masuala ya ulaji, kwanza unapokula hakikisha kwamba unachoma 'Carlolis' ambazo umezipata na kiukweli hakuna njia ya mkato , wewe umejenga mwili kwa muda mrefu halafu unataka siku moja uamke ukute umekonda ni kitu ambacho hakiwezekani.

"Wengi wetu tunadanganyana na inafika mahali tunaacha kula unashindia maji tu ,ni kwamba hapo unatengeneza tatizo jingingine kwasababu mwili jinsi ulivyo ili mifumo yako yoote ifanye kazi vizuri inatakiwa kuwa na kiasi cha virutubisho ambazo mwili unatakiwa upate kila siku ili mifumo iweze kujengeka vizuri.

"Ikitokea umekosa kitu tayari mwili unaanza kuleta shida,utafika mahali utaanza kuambiwa damu yako imepungua kwasababu kuna virutubisho hukuvipata vizuri mwilini , utafika mahali utaona mifumo inaanza kukataa , wengine tunafika mahali si unaona hata sasa hivi heshima inakuwa haipo,saa zingine ukiacha matatizo mengine pia na hizi staili na ulaji wetu unachangia.

"Tunakosa vile virutubisho vya msingi kwa ajili ya kuufanya ule mfumo ufanye kazi vizuri,kwa hiyo ukifika mahali unataka kuupunguza mwili kwa haraka kwamba nimeamua sili ila nakunywa maji ujue kabisa unakoelekea utapunguza baadhi ya virutubishi na wewe utaona mwili umepungua lakini unatengeneza madhara mengine mwilini,"amesema Dk.Grace.

Ameongeza kuwa kwa hiyo sio sawa na kwamba Kama unajua mwili umeujenga kwa muda mrefu hivyo hata kuupunguza kwake itachukua muda, hivyo unachotakiwa ni hakikisha unachoma Carlolis wakati unakula chakula ambacho kiko balansi."Balansi kwa maana ya kupata chakula chenye virutubisho vyote vinavyohitajika mwilini kwa ajili ya kufanya mifumo yako ifanye kazi mwilini vizuri."

Kuhusu mazoezi amesema walio wengi wanakosea."Unakuta inapigwa kampeni ya mazoezi sawa, tunakimbia Viwanja vya Leaders , tunafanya mazoezi ya nguvu ,unajua mwill unatabia moja ukichoma zile Carlolis halafu ukaziongeza kwa nguvu mwili unaongezeka kwasababu si umetengenezwa nafasi ,kwa hiyo nafasi yote inajaziwa.

"Kwa hiyo utaona umefanya mazoezi lakini ndio unatengeneza mwill zaidi.Lakini tunapiga kampeni tunakwenda Leaders Jumamosi tunakimbia weee tukimaliza pale pale pembeni kuna mgaha wameweka chapati tatu na supu yenye mafuta ,kwa hiyo unatoka pale umeshachoma Carlolis vizuri ...

"Lakini unakwenda kuharibu zaidi kwasababu umetengenezwa nafasi katika mwili halafu umeenda kujazia yaani umeharibu zaidi kwa hiyo unajikuta hata yale mazoezi hayakusaidii,kwa hiyo mazoezi lazima yaende sambamba na namna unavyokula."
MWENYEKITI  wa Shirikisho la Vyama vya Magonjwa Yasioambukiza  (TANCDA) Prof. Andwer Swai akitoa mada ya  ugonjwa wa kisukari kwa washiriki wa mkutano wa kuwajenga uwezo wa kuyafahamu magonjwa yasiyoambukiza.






Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2