Mkurugenzi Mtendaji Vodacom Tanzania PLC azuru vyombo vya habari vya IPP Media, Mwananchi Communications Ltd na Clouds Media | Tarimo Blog

 

Mwenyekiti wa Clouds Media Group Joseph Kusaga (kushoto) akifanya mahojiano na Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania PLC, Sitholizwe Mdlalose kuhusu mipango-mkakati ya Vodacom kwa mwaka huu wa 2022 wakati Mkurugenzi huyo alipotembelea ofisi za Clouds Media na kupata fursa ya kujitambulisha kwa wafanyakazi chombo hicho.

Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania PLC, Sitholizwe Mdlalose akiwa kwenye chumba cha habari cha ITV na kufanya mahojiano wakati wa ziara ya Mkurugenzi huyo kwenye ofisi za IPP Media na kupata fursa ya kujitambulisha kwa wafanyakazi vyombo hivyo.
 Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania PLC, Sitholizwe Mdlalose (kulia) akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications Ltd, Bakari Machumu (kushoto)  Mkurugenzi huyo alipotembelea kwenye za Mwananchi  na kupata fursa ya kujitambulisha kwa wafanyakazi wa kampuni hiyo. Katikati ni  Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC , Rosalynn Mworia.

Meneja Matangazo EATV, Lidya Igarabuza (kushoto) akifanya mahojiano na Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania PLC, Sitholizwe Mdlalose kuhusu mipango-mkakati ya Vodacom kwa mwaka huu wa 2022 wakati wa ziara ya Mkurugenzi huyo mpya wa Vodacom kutembelea ofisi za IPP Media ambapo EATV/Radio ni mojawapo.

Mhariri Mkuu wa Gazeti la The Guardian, Wallace Maugo (kulia) akielezea namna ya uendeshaji wa kila siku wa gazeti hilo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Sitholizwe Mdlalose (wa tatu kulia) na Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC , Rosalynn Mworia (kushoto)

Mwenyekiti wa Clouds Media Group Joseph Kusaga (katikati) akimkaribisha Mkurugenzi wa Vodacom Tanzania PLC, Sitholizwe Mdlalose kwenye kipindi cha XXL Clouds Fm kinachoongozwa na Adam Mchomvu (kulia)




 
Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania PLC, Sitholizwe Mdlalose (wapili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa ITV/Radio One na Capital Tv/Capital Radio, Joyce Mhavile (wa pili kulia), Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Rosalynn Mworia (kulia) na Mkurugenzi wa Masoko wa ITV/Radio One na Capital Tv, Joyce Luhanga, mara baada ya Mkurugenzi mpya wa Vodacom kutembelea ofisi za IPP Media na kupata fursa ya kujionea utendaji kazi pamoja na kujitambulisha kwa wafanyakazi wa vyombo hivyo.



Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2