MBUNGE HAWA MCHAFU AELEZEA NAFASI YA BUNGE INAVYOWEZA KUISHAURI SERIKALI KUHUSU NCDs | Tarimo Blog



Na Said Mwishehe,Michuzi TV

KAMATI ya Masuala ya UKIMWI,Kifua Kikuu, Dawa za Kulevya na Magonjwa Yasioambukiza, ina nafasi kubwa katika kuisimamia na kuishauri Serikali kuhusu mambo mbalimbali ya kukabiliana na NCDs ikiwemo pamoja na kuishauri Serikali kuja na Sheria ya Masuala ya magonjwa yasiyoambikiza.

Hayo yamesemwa na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani Hawa Mchafu ambaye ni Mjumbe wa Kamati hiyo baada ya Michuzi Blog kutaka kufahamu nafasi ya wabunge katika kusaidiana na wadau mbalimbali kukabiliana na magonjwa yasiyoambikiza.

Amesema wakati umefika sasa kuwa na chombo au Tume itakayosimamia masuala na mambo yote yanayohusiana na NCDs yaani kama ilivyo TACAIDS katika katika kupambana na janga la UKIMWI."Ni muhimu kujua kwamba suala la NCDs ni suala mtambuka linacut cross katika wizara zaidi ya moja TAMISEMI, ipo kwa Waziri Mkuu, Miundombinu, Wizara ya Habari, Wizara ya Michezo, Wizara ya Fedha , Wizara ya Viwanda na Biashara , Wizara ya Elimu.

"Kwa ujumla wake ni wizara tofauti na taasisi tofauti tofauti hivyo Kamati yetu inayo jukumu la kuishauri Serikali kuja na MultiSector Approach ambayo wizara zote hizo kuzifanya ziongee lugha moja na kwenda na kutekeleza pamoja kuhusu suala zima la kukabiliana na magonjwa yasioambukiza isiwe kila Wizara inapanga vyake na kutekeleza kivyake au kila mmoja kupita njia yake, hakika tutachelewa kukabiliana na kumaliza changamoto za magonjwa yasioambukiza,"amesema.

Aidha amesema kwa upande Serikali na wadau mbalimbali wanalo jukumu la kutoa elimu, kujengea uwezo na kuielimisha jamii kuhusu masuala ya magonjwa yasiyoambukiza na gharama zinazotumika kugharamia kuwatibu wagonjwa hao sambamba na vifo vinavyotokana na NCDs.

Mbali na kuishauri Serikali pia Kamati yao wanayo nafasi ya kuishauri jamii kwa ujumla kubadili tabia juu ya mwendo wa maisha ikiwemo kuacha kula hovyo hususani vyakula vyenye chumvi nyingi, sukari nyingi , mafuta mengi na vyakula vya kusindika.Pia jamii inatakiwa kujikita kufanya mazoezi iwe ni sehemu yao ya maisha kwani inasaidia kujiweka katika hatari ya kupata magonjwa yasioambukizwa.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Pwani Hawa Mchafu Chakoma akizungumza nafasi ya Kamati ya Bunge inavyoweza kuishauri na kuisimamia Serikali katika kukabiliana na magonjwa yasiyoambikiza


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2