Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu na Tume ya Madini waendesha Operesheni ya wasafirishaji wa Mchanga | Tarimo Blog


*Magari sita yanaswa watakiwa kulipa faini ya kufanya biashara hiyo bila kibali

Na Chalila Kibuda, Michuzi TV

Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu na Tume ya Madini wameendesha operesheni ya pamoja ya kuwasaka watu wanaofanya biashara ya mchanga bila kibali katika Mto Mpiji pamoja na Tegeta na kufanikisha kukamata magari matano.

Akzungumza katika Operesheni hiyo Kaimu Afisa Msaidizi wa Bonde la Wami/Ruvu Dar es Salaam Halima Faraj amesema kuwa magari waliyoyakamata wanatakiwa kulipa faini zilizowekwa kwa mujibu wa sheria.


Amesema hiyo biashara wanayoifanya ni katika mito ambayo haina vibali na kufanya uharibifu wa kingo za mito ambapo na kuharibu ikolojia ya mito.

Halima amesema kuwa operesheni hiyo ni endelevu na wanaofanya biashara hiyo wanatakiwa kubadilika kwa kufuata sheria za kukata vibali na bila kufanya hivyo biashara yao itakuwa ngumu kwani kila watapowakuta watawapiga faini na mwisho wa siku watataifisha magari.

"Biashara ya mchanga ambapo ni ndio madini inafanyika na ndio maendeleo lakini watu wafuate sheria na sio kufanya kama ni biashara ambayo haina msimamizi sasa hatuta waacha salama katika operesheni yetu" amesema Halima na kuongeza kuwa mbinu wanazotumia wanaofanya biashara ya madini hayo wanazijua hivyo hawana kwa kukwepea.

Nae Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Tume ya Madini Dar es Salaam Frank Simchile amessema kuwa biashara ya madini ya Mchanga wanatakiwa kufanya kwa kufuata sheria pamoja na utuzaji wa mazingira.

Simchile amesema kuwa baadhi ya watu walipewa vibali wameweza kupata miche ya kuzuia mmonyoko wa udongo lakini watu wasio na kibali wamekwenda kung'oa miche hiyo na kuchimba mchanga hali hiyo haiwezi kuvumiliwa na wafanyabiashara hao.

Aidha amesema kuwa wako macho kuhakikisha watu wanafuata sheria za mazingira pamoja na kuwa na vibali vya uchimbaji mchanga kwa maeneo yaliyoidhinishwa.

Kaimu Afisa Msaidizi wa Bodi ya Bonde la Wami/Ruvu Halima Faraji akizungumza katika MtoTegeta wakati wa operesheni ya wasafirishaji wa Madini ya Mchanga yanayotoka katika mto huo bila kibali nyuma yake ni gari lililokutwa likibeba mchanga ambapo wamelikamata kwa hatua za kisheria ,jijini Dar es Salaam.
Kaimu Afisa Msaidizi wa Bodi ya Bonde la Wami,Ruvu Dar es Salaam Halima Faraji akimsikiliza mwananchi katika operesheni ya wanasafirisha mchanga kutoka mto Tegeta.
Kaimu Afisa Madini Mkazi wa Tume ya Madini Dar es Salaam Frank Simchile akizungumza kuhusiana taratibu zilizoweka katika usafirishaji ya madini ya mchanga wakati wa Operesheni katika Mito jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya vijana waliokutwa wapakiaji mchanga katika mto Tegeta wakiwa chini ya Ulinzi




Baadhi ya magari yaliyokutwa yakibeba mchanga katika operesheni iliyofanyika katika Mito ya Jiji la Dar es Salaam.
 
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2