Janeth Raphael - MichuziTv DODOMA
Rais Samia anatambua juhudi zinazofanywa katika kuimarisha Amani nchini, kwa kushirikiana na Serikali hasa katika maeneo ambayo hayahitaji kutumiwa nguvu isipokuwa mazungumzo na maridhiano.
Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Hamad Masaun ameyasema hayo katika siku ya maadhimisho ya jumuiya ya maridhiano Tanzania yaliyofanyika jijini Dodoma
" Nchi ikitulia kama mnavyokusudia ni rahisi kupata maendeleo, nchi ikiwa na Amani ya kutosha ni rahisi kwa kila mtanzania kushiriki katika shughuli za maendeleo na katika kujenga uchumi wa nchi" - Masauni
Hata hivyo Waziri Masauni amewataka viongozi wa dini kuisaidia jamii kukabiliana na uhalifu ikiwamo swala la mauaji.
Amesema mauaji hayo yalijitokeza kati Januari na February mwaka huu 2022 yanachangiwa na sababu za kushangaza na za aibu kwa watu kujichukulia sheria mkononi kwa lengo la kujipatia mali.
Ametaja sababu nyingine ni wivu wa mapenzi, ramli chonganishi na ulevi wa kupindukia.
“Na ukifuatilia sababu gani zilizosababisha mauaji ni za kushangaza. Mfano wako watu ambao wamejichukulia sheria mkononi kwa kutafuta mali familia moja, ndugu kwa ndugu,”amesema.
Amesema wengine wanafanya mauaji kwasababu ya ramli chonganishi ambapo kuna makundi yamekuwa yakishiriki kuwapa watu wengine taarifa za uongo na kuhamasisha na kuchochea mauaji katika Taifa.
Hata hivyo Masauni amesema zipo changamoto ambazo jumuiya hiyo inaweza kukutana nazo katika utendaji wao, changamoto hizo zisiwakatishe tamaa katika Kufanya kazi zao na kuwasihi wasisite kushirikisha Serikali katika ngazi mbalimbali ili kwa pamoja changamoto hizo ziweze kutatuliwa na mwisho kufanikisha kujenga Tanzania iliyo Imara.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment