Ziara ya mwenyekiti wa wazazi taifa na mjumbe wa kamati kuu wa chama cha mapinduzi Dkt Edmund Mndolwa alisema katika ziara yake katika wilaya ya Namtumbo amefurahishwa na mapokezi mazuri yaliyofanywa na wanachama wa chama cha mapinduzi.
Dkt Mndolwa alidai amefurahishwa na mapokezi katika wilaya ya Namtumbo kutokana na kukutana na idadi kubwa ya wanachama waliokuwa na shauku ya kumwona na kumsikiliza hali iliyomfurahisha sana yeye akiwa wilayani hapo.
Mndolwa katika ziara hiyo aliwaambia wanachama wa chama cha mapinduzi wilaya ya Namtumbo kuwa kazi kubwa ya jumuiya ya wazazi ni pamoja na kuhamasisha swala la elimu nchini,kuhakikisha wazazi katika familia wanasimamia vyema malezi ya watoto wao pamoja na kuhakikisha jamii katika nchi hii wanalinda mazingira .
Akiongea na wanafunzi wa shule ya sekondari Luna iliyopo kata ya Luegu wilayani humo Dkt Mndolwa alisema wanafunzi kufeli mitihani ni mipango wanayojiwekea kwa kuwa wakiamua kufanya mitihani vizuri inawezekana kama wanaamua kufanya hivyo.
Aliwahatarisha wanafunzi kuacha kufanya urafiki na wanafunzi wenye ufaulu mdogo badala ya kufanya urafiki na wanafunzi wenye uwezo mzuri ili kuwafanya wenye uwezo mdogo kuweza kubaini mbinu zinazotumia na wenzao kufanya vizuri na kujibadilisha kimasomo badala ya kubaki na rafiki mwenya matokeo mabaya.
Aidha Dkt Mndolwa alifafanua swala la malezi ya watoto kwa kuwataka wazazi wenye watoto kuwalea watoto katika maadili mema ili kulijenga taifa lenye kuheshimu misingi iliyojengwa na waasisi wa taifa hili na kulinda tunu za taifa letu.
Hata hivyo Dkt Mndolwa alikemea wazazi wenye watoto wanaovuta bangi kuhakikisha wanarudi katika maisha yenye misingi bora na hasa kutumia makanisa na misikiti kupata malezi bora ya kiroho kwa kuacha mambo mabaya na kufuata mambo mema alisema Mndolwa.
Katika Hatua nyingine Dkt Mndolwa alidai wanachama na wananchi wa Tanzania wanatakiwa kulinda mazingira ili kuendelea kufaidi hali ya hewa iliyopo ambayo ni tegemeo kubwa kwa maisha ya binadamu na kuwahimiza wananchi kuhakisha kila mwananchi kupanda miti mitano kila mwaka ili kulinda mazingira yanayoharibiwa kwa kukata misitu laki nne kila mwaka.
Merina Victor katibu wa wazazi wa chama cha mapinduzi wilaya ya Namtumbo alitumia ziara hiyo kusoma taarifa ya ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa chama cha mapinduzi itakayotumia 22,825,500.mpaka kukamilika kwake.
Merina alidai nyumba imefikia katika hatua ya msingi ambapo ujenzi wa nyumba hiyo unategemea michango kutoka kwa wadau wakiwemo watumishi pamoja na wanachama wanaoguswa na swala hilo la ujenzi wa nyumba hiyo ya mtumishi wa chama.
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi mkoa wa Ruvuma Oddo Kirian Mwisho pamoja na mambo mengine alisema ziara ya Mwenyekiti wa Jumuiya ya wazazi taifa na mjumbe wa kamati kuu ya chama cha mapinduzi Dkt Edmund Mndolwa lengo lake kuu ni kukagua utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi katika ujenzi wa madarasa .
Ziara ya Dkt Edmund Mndolwa alikagua ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari Nasuli ,ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari Luna pamoja na kukagua ujenzi wa nyumba ya mtumishi wa chama cha mapinduzi wilayani humo na kufurahishwa na mapokezi yaliyofanywa kwake na chama wilayani humo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment