MRADI USINDIKAJI MATUNDA NA MBOGAMBOGA KUINUA UCHUMI HALMASHAURI MUHEZA | Tarimo Blog
Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza Amiri Msuya akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi wa Usindikaji wa Matunda na Mbogamboga ambao unatekelezwa na Taasisi ya Dira Women Organazation (DIWO) kwa kushirikiana na Stiftug Josef Vogt utawalenga vijana 150 wenye umri kuanzia miaka 16 hadi 24 ambao watatoka kwenye shule ya Sekondari Kicheba na vijana wanaoishi kwenye kata ya Kicheba.
Mkurugenzi wa Taasisi ya Dira Orgazation (DIWO) Shamsa Danga akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo kulia ni Diwani wa Kata ya Kicheba Mkodingwa kushoto ni Diwani wa Viti Maalumu Kibaha
Diwani wa Viti Maalumu Kibaha akizungumza
Diwani wa Kata ya Kicheba Mkodingwa akizungumza jambo kushoto ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Dira Orgazation (DIWO) Shamsa Danga
Diwani wa Kata ya Mlingano akizungumza jambo
NA OSCAR ASSENGA, MUHEZA.
MRADI wa Usindikaji wa Matunda na Mbogamboga umeelezwa kwamba utachangia kwa asilimia kubwa kuinua uchumi wa halmashauri ya wilaya ya Muheza kwa kukusanya ushuru wake na kuweza kuongeza wigo wa mapato ikiwemo kodi ya Serikali kuongezeka.
Mradi huo ambao unatekelezwa na Taasisi ya Dira Women Organazation (DIWO) kwa kushirikiana na Stiftug Josef Vogt utawalenga vijana 150 wenye umri kuanzia miaka 16 hadi 24 ambao watatoka kwenye shule ya Sekondari Kicheba na vijana wanaoishi kwenye kata ya Kicheba.
Utakwenda sambamba na utoaji mafunzo kwa vijana wa shule za Sekondari Kata ya Kicheba wilayani humo na kwa wale waliopo nje ya shule kuhusu masuala la ujasiriamali usindikaji wa mbogamboga ,usafi wa majumbani pamoja na utunzaji wa bustani.
Hayo yalisemwa na Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Muheza Amiri Msuya wakati uzinduzi wa mradi huo katika halfa iliyofanyika wilayani humo ambapo alisema ujio huo utawasaidia sana vijana kuweza kujikwamua kiuchumi ikiwemo kujiajiri.
Alisema baadaye wataona umuhimu na tija ya kuamua kuanzisha viwanda vidogo vidogo na Halmashauri kutokana na kupata fedha wanazokopeshwa kutoka kwenye mfumo wa vijana, wanawake na walemavu asilimia 10 za mapato ya ndani
Aidha alisema baada ya vijana hao kuweza kujua kuongeza thamani kwa mazao wanayosindika wanaamini watapata ajira na kupunguza wimbi la ambao hawana ajira kwa kuwa wataongeza thamani ya mazao na kuongeza kipato kwa mtu mmoja mmoja ikiwemo Halmashauri kuweza kukusanya ushuru na kuongeza mapato.
“Lakini kutokana na kuongeza thamani ya mazao Halmashauri itaongeza mapato kwani kuongezeka huko thamani itasaidia mazao yataweza kuonekana kwenye supermaketi na kuweza kuuzwa nje ya nchi na kipato kitapaa kwa sababu yale ambayo yalikuwa yakiharibika na kutupwa sasa yatakuwa yanauzika “Alisema
“Niwashukuru sana Taasisi ya Diwo ujio wenu hapa Muheza kwetu sisi ni kama Baraka na furaha kuona mnawasaidia vijana kwani kupitia mradi huu utawawezesha hata wanapopata mikopo ya vijana asilimia 4 kutoka Halmashauri wataweza kuwa wabunifu na kubuni miradi yenye tija”Alisema
Awali akizungumza wakati wa uzinduzi wa mradi huo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Dira Orgazation (DIWO) Shamsa Danga alisema mradi huo ni wa mwaka mmoja na upo kwa awamu tatu ambapo awamu ya kwanza itakuwa ni usindikaji wa matunda na mbogamboga.
Shamsa alisema awamu ya pili itakuwa ni utunzaji wa bustani na usafi wa majumbani ambapo unatajwa utakuwa mkombozi kwa vijana waliopo wilayani Muheza hususani Kata ya Kicheba ambapo utatekelezwa.
“Shughuli za mradi ni utoaji wa mafunzo kwa vijana juu ya usindikaji wa chakula kwa ajili ya uendelezi wa biashara kama njia na shughuli ya kujiingizia kipata na yatahusisha ujuzi wa ufungashaji na kuongeza thamani ya bidhaa zilizochaguliwa”Alisema
Alizitaja bidhaa hizo kama vile Tomato Sauce,Chill Sauce,Pactin,Jam ya fenesi,Juice ya fenesi,Viungo,Matunda yaliyokaushwa,Pickles,Fruits Jam,Crips na Pipi za maganda ya Machungwa”Alisema Mkurugenzi huyo.
Akieleza sababu za mradi huo kufanyika wilayani Muheza alisema kwa sababu ni eneo ambalo lilibarikiwa kuwa na matunda ya aina mbalimbali na mbogamboga pamoja na viungo.
Naye kwa upande wake Mwenyekiti wa Kijiji cha Kicheba B Rajabu Juma alisema wameipokea kwa mikono miwil taasisi hiyo ambayo imefika kwao wakati muafaka ambao watatoa mafunzo kwa vijana wao na kwamba wataiunga mkono kwa kuhakikisha hata pale panapohitajika shamba kwa ajili ya kilimo cha mbigambga halmashuri ya kijiji itakaa na kutoa ushikiri wa kulifanikisha hilo.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment