Na Mwandishi Wetu
UBALOZI wa Tanzania nchini Ufaransa kwa kushirikiana na taasisi ya kuendeleza sekta ya horticulture Tanzania (TAHA), umefanya Mkutano wa kutangaza fursa za bidhaa za matunda na mbogamboga (horticultural products) za Tanzania ili kuingia kwenye soko la nchi za Ulaya hususan Ufaransa.
Mkutano huo ulifanyika katika ukumbi wa Ubalozi na kuhudhuriwa na wafanya biashara wakubwa wa sekta hiyo. Katika mkutano huo, Mtendaji Mkuu wa (TAHA), Dkt Jacqueline Mkindi alielezea kuhusu ubora wa mazao kutoka Tanzania ambayo yanaweza kuuzwa katika soko la Ufaransa na la ulaya.
Katika taarifa yake, alisema kwamba tayari bidhaa nyingi zimeshaanza kuuzwa katika masoko mengi ya nchi za Ulaya na sasa anataka mazao hayo kuingia kwa wingi na kupata masoko nchini Ufaransa.
TAHA ilitia saini Mkataba wa Makubaliano (MOU) na kampuni ya Laparra ya Ufaransa, ambao ni waingizaji na wauzaji wakubwa wa mazao ya horticulture katika masoko ya Ufaransa. Makubaliano hayo yanalenga katika kutangaza na kuuza bidhaa (promotion and branding), katika masoko ya ndani na nje ya Ufaransa ikiwa ni mkakati wa kuendeleza sekta hiyo nchini Tanzania.
Kabla ya mkutano huo, Dkt Jacqueline Mkindi akiambatana na Mhe. Balozi Samwel W. Shekukindo, Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa walipata fursa ya kutembelea soko la kimataifa la Rungis (Soko kubwa kuliko yote la mazao ya kilimo katika bara la Ulaya).
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment