NACOPHA waishukuru serikali kwa kuendelea kutoa huduma za afya bure kwa WAVIU | Tarimo Blog





Njombe

Mkurugenzi msaidizi sera na mahusiano kutoka baraza la Taifa la watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI Tanzania NACOPHA Agnes Nyoni amemshukuru Rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania Samia Suruhu Hassani kwa kuendelea kutoa huduma za bure kwa watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi.

Mkurugenzi huyo ametoa shukrani hizo mbele ya waziri wa nchi,Ofisi ya Waziri mkuu Sera,Bunge na Uratibu balozi Pindi Chana katika ofisi ya mkuu wa mkoa wa Njombe ambapo alisema serikali inawajali na kuwathamini wanaoishi na virusi vya Ukimwi.

"Kwanza nichukuwe fursa hii kutoa shukrani za dhati kwa niaba ya baraza kwa mh Rais kwa kuendelea kutupa huduma hizi za VVU na Ukimwi bure bila ya malipo"amesema Agnes.

Mkurugenzi huyo amesema kwa upande wa mkoa wa Njombe wapo katika halmashauri sita ambazo zinatekeleza miradi ya muitikio wa Ukimwi.

Naye mwenyekiti wa jukwaa la wanawake waishio na maambukizi ya virusi vya Ukimwi Taifa Joselyn Mtono, ameishukuru serikali kwa kuendelea kutoa mikopo ya asilimia 10 kwa watu wanaoishi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi na kwamba fedha hizo zimeweza kuwaidia kuwainua kiuchumi.

Kwa upande wa waziri wa nchi,Ofisi ya Waziri mkuu Sera,Bunge na Uratibu balozi Pindi Chana amesema mkoa wa Njombe umefanikiwa kupunguza viwango vya maambukizi kwa watu wenye umri wa 15 hadi 49 vimepungua kutoka asilimia 14.8 mwaka 2012 hadi asilimia 11.4 mwaka 2017.

Hata hivyo waziri alipata fursa ya kutembelea shughuli mbalimbali za ujasiriamali na kulimo zinazofanywa na Watu wanaoishi na virusi vya Ukimwi.


 
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2