WANAWAKE TANESCO WAKABIDHI VIFAA VYA KUFUNDISHIA CHUO CHA UFUNDI ARUSHA (ATC) | Tarimo Blog




Na Mwandishi Wetu, Arusha .


KATIKA kuelekea siku ya wanawake duniani, Wafanyakazi wanawake wa Shirika la umeme Tanzania TANESCO kupitia tawi la TUICO Makao Makuu wameadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kutoa msaada wa vifaa vya kufundishia umeme katika Chuo cha Ufundi Arusha ATC.

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Machi 5,2022 Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha John Mongela amesema “ninawapongeza sana wanawake wa TANESCO kwa kutekeleza jambo hili lenye lengo la kuwapa hamasa mabinti waliopo vyuoni kusoma kwa bidii.”

Mongela ameongeza kuwa Serikali ya Awamu ya sita chini ya uongozi thabiti wa Rais mama Samia Suluhu Hassan unafanya jitihada kubwa katika kuboresha mazingira ya utoaji elimu. "Na inapotokea taasisi za umma zikaunga mkono jitihada hizo kwa kuchangia uboreshaji elimu kunawezesha watoto wengi zaidi kufikiwa na huduma za elimu.

"Hivyo niwasihi TANESCO msiishie Chuo cha ufundi Arusha pekee bali mtembelee na maeneo mengine yenye changamoto na kuwasaidia kama nafasi yenu kushirikiana na jamii zinazo wazunguka.kwadababu TANESCO inatoa huduma zake nchi nzima.

" Kutoa msaada wa vifaa vya kufundishia katika Chuo cha ufundi Arusha kutawapa hamasa wanafunzi wa kike wanaochukua masomo ya ufundi chuoni hapa hasa ikizingatiwa kuwa wameona shuhuda za wanawake wa TANESCO walio soma hapa na serikali kuwaajiri katika shirika letu la umeme. Na kupata nafasi ya kuongoza mikoa mbalimbali na vitengo maalum katika shirika."

Kwa upande wake Mhandisi Sophia Mgonja ambaye ni Mwakilishi wa wanawake wa TANESCO makao makuu amesema lengo la wanawake hao kufika katika chuo hicho ni kuhamasisha mabinti wanaosomea masomo ya ufundi umeme kufanya bidii katika masomo yao ili na wao waje kupata nafasi za ajira katika shirika letu na kuendeleza pale ambapo wanawake hao wataishia.

Mhandisi Mgonja ameongeza ni wakati wa mabinti kuongeza juhudi na uadilifu na kufaulu vizuri ili waje kuwa mafundi bora watakao endeleza miradi mbalimbali ambayo serikali inaitekeleza.

Sambamba na kukabidhi msaada wa vifaa hivyo,wanawake wa TANESCO Makao makuu pia wameendesha harambee ya kuchangia fedha kwaajili ya kusomesha wanafunzi wa kike walio katika mazingira magumu na kukosa ada ili waweze kukamilisha masomo yao ambapo zaidi ya Shilingi milioni moja zilipatikana na kufanikisha kulipa ada ya mwaka kwa mwanafunzi aliyetaka kukatisha masomo.


Mhandisi Sophia Mgonja ambaye ni Mwakilishi wa Wanawake wa TANESCO  makao makuu akikabidhi vifaa vya kufundishia umeme kwa wanafunzi katika chuo cha ufundi Arusha.

Mkuu wa mkoa wa Arusha  John Mongela akiwa katika picha ya pamoja na wanawake wa TANESCO  makao makuu walio tembelea  chuo cha ufundi  Arusha
 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2