Janeth Raphael - MichuziTv Dodoma
Zikiwa zimebaki siku chache kuadhimisha siku ya Wanawake duniani imezoeleka wanawake hao kutoka maeneo mbali mbali kote duniani hujitokeza na kufanya Shughuli zinazogusa jamii ili kuikumbuka siku hiyo muhimi ambayo huadhimishwa kila ifikapo tarehe 8 mwezi wa 3 kila mwaka.
Kwa kulitambua hilo wanawake wa Mamlaka ya majisafi na Mazingira Dodoma (DUWASA) wametembelea kituo Cha watoto walemavu kilichopo kijiji cha Mlali Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma na kuwapa faraja watoto hao wanaoishi katika Mazingira magumu.
Akizungumza Mara baada ya kufika katika kituo hicho na kujionea hali halisi ya watoto hao Katibu wa kina mama hao wa Duwasa Mkoa wa Dodoma Esther Mlewa amesema wametembelea kituo hicho kwa kuwa watoto hao ni sehemu ya wanaohitaji msaada hivyo kwa kushirikiana na Mkurugenzi Mtendaji wa DUWASA na wafanyakazi wote walikaa na kuona Kuna haja ya wao Kama wanawake wa ofisi hiyo kushiriki jambo hilo katika moja ya kituo cha watoto hao wenye mahitaji maalumu.
" Kutembelea vituo vya watoto wenye mahitaji Kama hawa ni sadaka kila mmoja wetu amejitahidi kubeba sadaka aliyonayo kadri Mungu alivyomuwezesha na tumekuja kuwapa faraja watoto hawa na kila mama amebeba kitu chake binafsi kuwa ajili yao" - Amesema Esther.
Esther amesema wao kama DUWASA wamejifunza vitu vingi sana kwa kuwa wanapokuwa huko mjini au hata nyumbani siyo rahisi kufahamu umuhimu wa watoto kuhitaji misaada katika vituo mbalimbali lakini unapopata nafasi ya kuwatembelea watoto wenye uhitaji kweli kuna la kujifunza sana na amewashauri hasa kina mama wajitokeze kwa wingi kutembelewa vituo mbalimbali nchini ili watoto wanaolelewa huko wapate faraja Mana Kufanya hivyo ni ibada.
Naye Mkurugenzi wa kituo hicho Padri Gaudence Aikarua amesema watu kuficha watoto ndani ni changamoto kubwa hivyo wanatakiwa waamke na kuacha mila hizo potofu za kuwaficha watoto walemavu ndani, wawatoe watoto hao katika vituo ili wapate matibabu Mana wengine viungo vyao vinapona kabisa na kuendelea na maisha kawaida.
"Kuna matatizo mengi yanaachwa na kuja kuwa makubwa bila sababu Mana yakiwahiwa yanaweza kushugulikiwa na walemavu hao wakajerea katika viungo vyao vya kawaida" - Amesema Padri Aikarua.
Padri Aikarua amewaomba wazazi pamoja na jamii kwa ujumla waache hizo tabia za kuficha watoto au watu wenye ulemavu mana wanasababisha kuua ndoto nyingi za vijana wa taifa la kesho na bado walemavu hao ni zawadi kutoka kwa Mungu hivyo hawapaswi kufichwa na kuona hilo ni jukumu la kila mmoja wao.
Kwa upande wake Daktari wa kituo hicho Hillary Senga amesema kituo hicho kinapokea watoto wenye ulemavu tofautitofauti lakini zaidi wanawachukua wale wenye utindio wa ubongo na wanahitaji ukaribu zaidi wa kitabibu
"Watoto hawa wanahitaji kuangaliwa kwa jicho la ukaribu sana kutokana na afya zao mana pia Wana changamoto za kupata degedege Mara kwa mara hivyo kama Dakitari napaswa kuwa hapa kituoni muda wote" - Dkt Senga
Dkt Senga amesema inahitajika Elimu ya kutosha kwa wazazi wa watoto wanaozaliwa na changamoto hizo ili kutambua mtoto huyo anapokuja duniani akiwa na ulemavu huo anapelekwa wapi hasa ili kupata matibabu mana taasisi nyingi hazifanyi matangazo juu ya maswala hayo hivyo mabalozi wengi wanahitajika kupaza sauti mana ulemavu si kifo Mara nyingi wanatibiwa na kurudi katika hali zao za kawaida.
Hata hivyo mmoja wa wazazi ambaye mtoto wake analelewa katika kituo hicho Magdalena Gombanila amesema anawashukuru watendaji wote wa kituo hicho kwa kuwa wanapata huduma nzuri watoto wengi wanafika kituoni hapo wakiwa na hali mbaya Sana lakini kupitia wao watoto wanapona na wengi wao wanarejea majumbani wakiwa na afya nyema.
" Nawasihi wazazi wenzangu ambao Wana watoto walemavu Kama huyu wakwangu wasiwafiche watoto wao nyumbani wajitokeze na watoto wao watapata huduma na kuwarejeshea matumanini ya maisha yao" - amesema Magdalena.
Wakati huo huo amewashukuru Wanawake wa DUWASA kwa kuwatembelea Mana wamewapa faraja na kuwatia moyo sana, amewaomba waendelee na moyo huo huo mana watoto wanahitaji faraja sana.
Katibu wa kina mama wa Mamlaka ya maji safi na mazingira Dodoma ( DUWASA Esther Mlewa akizungumza na waandishi wa habari ( hawapo katika picha)
Mkurugenzi Mtendaji kituo Cha watoto walemavu Mlali Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma akizungumza jambo
Mkurugenzi wa kituo Cha watoto wenye ulemavu Mlali Padri Gaudence Aikarua akiteta jambo na kina mama wa DUWASA
Wanawake wa DUWASA wakila pamoja na kuwafariji watoto walemavu wanaolelewa katika kituo Cha Mlali Wilaya ya Kongwa Mkoani Dodoma
Katibu wa wanawake wa Mamlaka ya majisafi na Mazingira Esther Mlewa akiwa na mmoja wa watawa wa kituo hicho
Wanawake wa DUWASA wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya watoto Mara baada ya kukabidhi misaada mbalimbali kwa watoto hao
Dkt Hillary Senga ambaye ndiye Dakitari mkuu anayewatibu watoto wa kituo hicho cha Mlala, Kongwa Mkoani Dodoma.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment