ZAIDI YA WANANCHI 22,000 WA NYANGAO - MTAMA KUPATA MAJI SAFI NA SALAMA | Tarimo Blog


Mbunge wa Jimbo la Mtama na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye ameshuhudia utiaji saini wa mkataba baina ya Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) wa Mkoa wa Lindi na mkandarasi wa Kampuni ya Halem Construction Limited kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya maji safi na salama wa mradi wa Nnyangao - Mtama

Ujenzi wa mradi huo utanufainisha na kuwawezesha wananchi zaidi ya 22,000 kupata maji safi na salama ambao utagharimu zaidi ya shilingi 4,577,244,446

Mradi huo utatekelezwa jimboni humo  kwenye kata tatu za Majengo, Mtama na Nyangao zenye jumla ya vijiji 13    vya Nyangao A,  Nyangao B, Mtakuja II, Nangaka, Masasi, Majengo A, Majengo B, Mvuleni, Mihogoni, Mbalala, Makonde, Mnamba (Chluwe) na Mkwajuni

Viongozi wengine walioambatana na Mhe. Waziri Nape  ni Mhe. Shaibu Issa Ndemanga, Mkuu wa Wilaya Lindi; Mhe. Yusuph Abdalah Tipu, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mtama; Waheshimiwa madiwani wa maeneo husika, watendaji wa Ruwasa na Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya wakiongozwa na Mwenyekiti  comred Athumani Seif Hongonyoko.

Waziri Nape amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo kwa ajili ya ujenzi wa mradi huo.

Mbunge wa Jimbo la Mtama na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akishuhudia utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa mradi wa maji safi na salama baina ya RUWASA na mkandarasi wa Kampuni ya Halem Construction Ltd kwa ajili ya kufikisha huduma ya maji kwenye kata tatu za jimbo hilo
Mbunge wa Jimbo la Mtama na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye akifurahia na baadhi ya Wananchi wa jimboni kwake mara baada ya kushuhudia  utiaji saini wa mkataba wa ujenzi mradi wa maji safi na salama baina ya RUWASA na mkandarasi wa Kampuni ya Halem Construction Ltd kwa ajili ya kufikisha huduma ya maji kwenye kata tatu za jimbo hilo
 



Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2