Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Alhajj Abdulrahman Kinana, amejumuika na viongozi mbalimbali wakiwemo wa dini, wa serikali na Chama, mkoani Arusha, katika futari aliyowaandalia.
Kinana alifutari na wananchi hao leo April 26, 2022 katika Ofisi za CCM Mkoa wa Arusha ambapo miongoni mwa walioshiriki ni Katibu wa NEC ya CCM Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka na viongozi wengine wa serikali.
Akitoa shukrani kwa niaba ya Alhajj Kinana, Shaka alisema kitendo cha kujumuika pamoja katika futari hiyo kinaonesha ushirikiano na mshikamano ambao unapaswa kupendekezwa na Watanzania.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment