BABA WA KAMBO ADAIWA KUMCHEZEA SEHEMU ZA SIRI MTOTO WA MIEZI 11 TANGA | Tarimo Blog

 Raisa Said,Tanga

Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 26 anashikiriwa na Jeshi la Polisi Mkoani Tanga Kwa tuhuma za kumpenyezea vidole sehemu za Siri mtoto mwenye umri wa miezi 11 ambaye  ni mtoto wake wa kambo.

Akizingumza na Waandishi wa Habari Kamanda wa Polisi Mkoani hapa Safia Jongo amesema wanamshirikia mwaume huyo kwaajili ya uchunguzi wa tuhuma zinazomkabili.

Kamanda Jongo amesema kuwa mwanaume huyo Mkazi wa Mikocheni  eneo la amboni anatuhumiwa kufanya tukio hilo April  11 mwaka huu  nakuongeza kuwa alifanya tukio Kwa mtoto huyo aliyekuwa amebebwa  mgogongoni na Mama yake ambaye ni mkewe .

Amesema kuwa inadaiwa mwanaume huyo amezoea kumfanyia mtoto huyo kitendo hicho Cha kinyama jambo lililopelekea Mama Mzazi wa mtoto huyo kufika Kituo Cha Polisi kutoa taarifa.

" Mama Mzazi wa mtoto huyo alibaini kuwepo Kwa vitendo hivyo visivyo vya kawaida  Kwa mtoto wake baada ya mtoto kuwa kuanza tabia ya kulia na kutoa harufu mbaya sehemu zake za Siri" amesema  Kamanda Jongo.

Hata hivyo Jongo emeeleza kuwa uchunguzi wa Daktari umethibitisha ni kweli sehemu za Siri za mtoto huyo zipo wazi japo hajaingiliwa  kimwili lakini zipo wazi inamaana yule mtoto alikuwa akichezewa Kwa muda mrefu.

Baadhi ya Wakazi wa Amboni anakokaa mwanaume huyo wamelipongeza Jeshi la Polisi Kwa kumkamata mwanaume huyo ambapo wa meshauri kwamba akithibitika Sheria ifuate mkondo wake.

Mwanakombo Jumaa Mkazi wa Tanga yeye ameenda mbali zaidi Kwa kusema kuwa huyo mwanaume anaweza kuwa akili zake haziko sawa au anafanya hivyo Kutokana na imani za kishirikina.

Hata hivyo kufuatia program jumuishi ya malezi ,Makuzi na Maendeleo ya awali ya mtoto inaeleza kuwa katika vitendo vya ukatili wa watoto kuna upungufu wa utoaji taarifa za kesi za unyanyasaji na utelekezaji watoto kuanzia miaka 0 mpaka minane ambapo kwa utafiti uliofanywa na Benki ya Dunia katika mkoa wa Katavi umeonyesha asilimia 18 ya wazazi wenye watoto chini ya miaka mitatu kuwapiga vibao watoto wao.

Hata hivyo katika kukabiliana na vitendo  vya ukatili dhidi ya watoto  na wanawake ,Serikali iliandaa mpango kazi wa Taifa wa kutokomeza  ukatili dhidi ya Wanawake na watoto  wa mwaka 2016/2017- 2021/22 (Mtakuwa ). mpango huu jumuishi unalenga kutokomeza ukatili  Kwa kina  ukiwa na afua ambazo zimelenga elimu ya malezi ,usalama.shuleni , utekelezaji wa Sheria ,mazingira salama katika maeneo ya umeme na maeneo mengine.



Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2