BODI YA USHAURI TARURA YAFANYA UKAGUZI UJENZI WA BARABARA KATIKA MJI WA SERIKALI MTUMBA | Tarimo Blog

Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA imefanya ukaguzi wa  mradi wa ujenzi wa Barabara za Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma  unaotekelezwa na Mkandarasi China Heinan International Group Co Ltd (CHICO) ambapo kwa awamu ya kwanza mradi huo umekamilika kwa asilimia 100.

Akizungumza katika ukaguzi huo Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TARURA Mhandisi Florian Kabaka ameeleza kazi ziliyofanyika ni nzuri huku akitoa wito kwa wananchi kuhakikisha wanalinda miundombinu ya barabara ili iweze kutumika kama ilivyokusudiwa.

‘‘Tumebaini changamoto baadhi ya watu wasio waaminifu kuiba miundombinu ya barabara zikiwemo taa, suala hili  halipendezi, natoa wito kwa Menejimenti kuwasiliana na Serikali ya Mkoa, Wilaya pamoja na Kata ili kuweka mikakati wa kulinda miundombinu hii na kuchukua hatua kali kwa watakaobainika  kuhujumu barabara hizi’’, alisema Mhandisi Kabaka.

Naye Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA Mhandisi Victor H. Seff alisema awamu ya kwanza ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami zenye urefu wa Kilomita 51.2  katika Mji wa Serikali Mtumba tayari imekamilika na sasa Mkandarasi ameanza awamu ya pili itakayo husisha ujenzi wa barabara za mlisho zenye urefu wa kilomita 7.91.

‘‘Awamu hii ya pili ya ujenzi wa Barabara za Mlisho zenye urefu wa kilomita 7.91 utatumia muda wa miezi 8 hadi kukamilika ambapo hadi sasa tayari Mkandarasi yupo Site”.

Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini TARURA unaendelea kutekeleza miradi mbalimbali nchini ikiwa ni pamoja na kufungua barabara kuwezesha wananchi kufika kusiko fikika.

Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya TARURA Mhandisi Florian (wa tatu kulia) Kabaka pamoja na wajumbe wa Bodi  wakipata maelezo kutoka kwa Mratibu wa Mradi wa ujenzi wa Barabara za Mji wa Serikali Mtumba Mhandisi Benjamin Magege wakati wa ziara ya ukaguzi wa mradi huo, jijini Dodoma.

Mtendaji Mkuu wa TARURA Mhandisi Victor H. Seff akitoa maelezo kwa wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya TARURA kuhusu ujenzi wa Barabara katika Mji wa Serikali Mtumba wakati wa ziara ya ukaguzi wa mradi huo, jijini Dodoma.



Mratibu wa mradi wa ujenzi wa Barabara katika Mji wa Serikali Mtumba Mhandisi Benjamin Magege akitoa maelezo kuhusu mradi huo kwa Wajumbe wa Bodi ya Ushauri ya TARURA wakati wa ziara ya ukaguzi wa mradi jijini Dodoma.

 


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2