Na mwandishi wetu
Ubalozi wa Tanzania - Paris, unaowakilisha pia Tanzania katika nchi ya Uhispania umefanya hafla fupi ya chakula cha mchana pamoja na uongozi na vijana wanaochipukia kwenye mchezo wa mpira wa miguu ambao wanaendelezwa vipaji vyao na Kituo cha Magnet Youth Academy cha mjini Dar es Salaam.
Hafla hiyo ilifanyika mjini Madrid wakati wachezaji hao walipowasili kutokea jijini Celta Vigo walikokwenda kwenye majaribio ya kucheza soka.
Akizungumza na wachezaji na uongozi, Balozi wa Tanzania nchini Uhispania mwenye makazi yake mjini Paris, Mhe. Balozi Samwel W. Shelukindo aliwapongeza wachezaji hao kwa vipaji vyao na kuwatia moyo kuendelea zaidi ili waweze kupeperusha bendera ya Tanzania katika siku zijazo.
Vile vile alikipongeza kituo hicho kwa malezi bora ya vijana katika mchezo wa soka. Alisema Ubalozi uko tayari kuwasaidia wakati wowote watakapohitaji kufanya hivyo.
Naye Kiongozi wa klabu hiyo Bw. Tuntufye Mwambusi
alisema, vijana hao wadogo wameonyesha vipaji vya hali ya juu wakati wa mafunzo waliokuwa wakipewa na Kituo cha Celta Vigo.
Bw. Mwambusi alisema vijana wawili kutoka kituo chake watabaki mjini Madrid kwa siku chache kwa ajili ya kucheza mechi za majaribio.
Aidha, aliushukuru Ubalozi kwa mapokezi mazuri mjini Madrid na kuahidi kuendelea kushirikiana na Ubalozi katika kuendeleza mchezo wa soka kwa vijana.
Balozi wa Tanzania nchini Uhispania mwenye makazi yake mjini Paris akiwa katika picha ya pamoja na vijana wa kitanzania waliokwenda nchini Uhispania kwa majaribio ya kucheza soka. Kutoka kulia ni Joseph jr ,Ethan Fredrick na Troy Makoi, na upande wa kushoto ni Abdul Mandeke, Patrick Elijah, Ahmed Pipino (Diego), Avner Mlina, Samuel Shilla, Lenox Mgitu
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment