MFANANO WA WAFUNGWA ULIVYOPELEKEA UGUNDUZI WA ALAMA ZA VIDOLE 'FINGERPRINT' | Tarimo Blog



Na Leandra Gabriel, Michuzi TV


BAADA ya Willium West Mmarekani mwenye asili ya Afrika kuhukumiwa kifungo cha maisha kwa kosa la mauaji anatokea mfungwa mwingine mwenye jina la Will West aliyefanana na mtuhumiwa wa kwanza kwa sura, miaka, umbo, urefu na miaka.

Mei Mosi, 1903 nchini Marekani mwanaume mmoja Mmarekani mwenye asili ya Afrika aliyefahamika kwa jina la Will West alipelekwa katika gereza la Leavenworth, akiwa mfungwa mpya katika gereza hilo Will aliwekwa katika utaratibu wa kawaida ikiwemo kupigwa picha pamoja na kuchukuliwa maelezo ya mwili pamoja na vipimo 11 zaidi na makarani wa gereza hilo.

Kwa maelezo na picha zilizochukuliwa kutoka kwa Will makarani waligundua kuna mfanano mkubwa na Willium West ambaye rekodi zilionesha awali alikuwa na hatia ya mauaji na alikuwa akitumikia kifungo cha maisha, licha ya kuoneshwa picha na maelezo hayo kutoka kwa makarani Will West alikanusha kuwa hakuwa mtu huyo na hakuwahi kufungwa katika gereza lolote.

Baada ya Maofisa wa Polisi kuchukua maelezo ya Willium West aliyekuwa akitumikia kifungo ikiwa anafahamiana na Will West alikana kabisa kufahamiana na mtu huyo waliyeonekana kama mapacha na hata walipokutanishwa walishangaa kwa namna walivyofanana, hapo ndipo teknolojia ya kutumia alama za vidole 'Fingerprint' iliibuka kwani watu hao walifanana kwa kila kitu lakini alama za vidole vyao 'Fingerprint' hazikufanana.

Kesi ya wawili hao ilipelekea kuibuka kwa teknolojia ya alama za vidole 'Fingerprint' na utambuzi kuanza kufanywa kwa kutumia alama za vidole. Ikumbukwe kuwa kwa wakati huo teknolojia pekee iliyokuwa ikitumia kuwatambua wahalifu ilikuwa ni 'Bertilion measurement' ambayo ilihusisha kupima muonekano wa mtu.





Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2