BANK YA EQUITY YALETA WAWEKEZAJI KUTOKA MAREKANI WAJADILI FURSA ZA UWEKEZAJI | Tarimo Blog

 

Mkurugenzi wa Sera, Utetezi na Usimamizi wa Uanachama wa TPSF, Zachy Mbenna akizumgumza na waandishi wa habari wakati wa Ufunguzi wa Ufunguzi wa Ujumbe wa Biashara ya Marekani nchini Kenya na Tanzania unaofanyika jijini Dar Es Salaam. Hafla hii imeandaliwa na Benki ya Equit Tanzania.
Baadhi ya wawekezaji kutoka  nchini Marekani wenye nia ya kuwekeza nchini Tanzania na Kenya waliotoka katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, kilimo, usafirishaji n.k ambayo imeratibiwa na Benki ya Equity
Adams marandu akizumgumza na waandishi wa habari wakati wa Ufunguzi wa Ufunguzi wa Ujumbe wa Biashara ya Marekani nchini Kenya na Tanzania unaofanyika jijini Dar Es Salaam. Hafla hii imeandaliwa na Benki ya Equit Tanzania.

Na Mwandishi wetu
BENKI ya Equity imeendelea kuhakikisha wawekezaji kutoka nje wanakuja nchini kuwezekeza ili kuwawezesha wafanyabishara nchini kupata nafasi ya kukuza soko kwa kuuza bidhaa zao lakini pia kupata kuungana na wanunuzi katika maeneo mengine.

Hayo aliyasema Mwangalizi wa biashara kutoka Benki ya Equity, Adams Marandu wakati akizungumza na waandishi wa habari katika ziara ya kimkakati iliyofanywa na wawekezaji kutoka nchini Marekani wenye nia ya kuwekeza nchini Tanzania na Kenya waliotoka katika sekta mbalimbali ikiwemo afya, kilimo, usafirishaji n.k ambayo imeratibiwa na Benki ya Equity.

"Tutaendelea kuhakikisha fursa za kilimo, uwekezaji, logistics zinakua explode kwa ukubwa wake kulingana na tanza ilivyokuwa potential recorded kama ilivyo Afrika"

Aidha Marandu alisema Kumekuwa na changamoto kabla na baada ya Covid -19, hivyo kutoka na changamoto hizo kama Benki ya Equity wanaiona Afrika na Tanzania kama kuna nafasi kubwa sana ya kuwa kikapu cha chakula cha Dunia ndiyo maana wanawashirikisha wawekezaji kutoka Duniani lakini pia Afrika wanaozunguka kutoka Tanzania ili kuja kufanya uwekezaji.

"Tanzania ina eneo kubwa la Ardhi, nafasi kubwa ya vyanzo vya umwagiliaji kutokana na hilo, tunashirikisha wawekezaji kutoka Duniani lakini pia kutoka Afrika wanaotuzunguka kutoka Tanzania" alisema Marandu

Kwa upande wake Mkurugenzi kutoka Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania, Zack Mbena amewataka wafanyabishara nchini kutumia vizuri fursa hiyo ya wawekezaji kutoka Marekani waliokuja nchini ili biashara zao kuwa na viwango lakini pia kuleta teknolojia hasa katika maeneo ya viwanda , TEHAMA na sekta ya huduma za kifedha.

"Kufanya biashara ya kimataifa inahitaji viwango vya kimataifa hivyo watanzia na makampuni ya Tanzania yatanufaika kupata hivyo viwango kwa kushirikiana na wafanyabishara wawekezaji ambao wamekuja lakini pia watasaidia kuleta teknolojia hasa katika maeneo kama ya viwanda vya kutengeneza dawa, TEHAMA na sekta ya huduma za kifedha"

Mbena alisema Wafanyabishara hao kutoka nje wanania ya kuwekeza katika sekta ya utalii ambapo wameonyesha nia ya kujenga hoteli mbalimbali na kuanzisha makampuni ambayo yataleta watalii hapa nchini hivyo amewataka watanzania kutumia nafasi hiyo ili kutatua changamoto ya mitaji ambayo imekuwa ikijitokeza nchini.

"Kwa makampuni ya kitanzania pia ni nafasi, tumekuwa na changamoto ya kupata mitaji, sasa hawa wafanyabishara wa nje wanaleta mitaji hivyo ni vyema waweze kufika katika jukwaa la uwekezaji waongee nao, waweze kupata nafasi ya kubadilishana mawasiliano lakini pia walete mawazo yao ya kibiashara"

Pia alisema Kwa upande wa wafanyabishara wa Tanzania wanapenda kufanya biashara katika maeneo ya viwanda na kilimo ambapo wanalenga kuchukua mazao yanayopatikana Tanzania na kufanya Tanzania kuwa kikapu au kituo cha bidhaa za kilimo ambazo zitaenda Marekani na masoko mengine ambayo yanazunguka.

alisema Ziara za wawekezaji ni kazi nzuri ambayo inafanywa na serikali ya jamuhuri ya muungano wa Tanzanzia chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ambapo amekuwa mstari wa mbele kuifungua nchi kukaribisha uwekezaji kufiatia ziara yake ya Marekani ambayo ilikuwa ni sehemu ya mchango katika kuwaleta wawekezaji hao kutoka Marekani.

Kwa upande wao baadhi ya wawekezaji walioshiriki katika mkutano huo wamesema kuwa Tanzania imekua ni kitivo na mlango wa uwekezaji kutokana na sera na mazimgira yake yaliyopo,hivyo wanavutiwa kuwekeza katika nchi ambayo wana uhakika itazaa matunda katika uwekezaji wao.

Mkurugenzi wa Sera, Utetezi na Usimamizi wa Uanachama wa TPSF, Zachy Mbenna akitoa taarifa kwa waandishi wa habari wakati wa Ufunguzi wa Ufunguzi wa Ujumbe wa Biashara ya Marekani nchini Kenya na Tanzania unaofanyika jijini Dar Es Salaam. Hafla hii imeandaliwa na Benki ya Equit Tanzania.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2