Na Mwandishi wetu
MAFUNDI Ujenzi asilimia 59.5 hawajajiunga na kikundi chochote huku asilimia 40.5 tuu ndio wamejiunga hiyo imedhiirika katika mkutano ambao chuo Kikuu Mzumbe walikuwa wanasambaza matokeo ya Utafiti juu ya Sekta ya Ujenzi na Manufaa ya Mafundi Ujenzi Katika Huduma za Hifadhi ya Jamii.
Na Asilimia asilimia 85.9 ya wajenzi utafiti umeonesha kuwa hawana bima huku asilimia 14.1 tu ndio wamejiunga na bima ya afya wakati kati ya hao asilimia 94.1 wanauelewa na elimu juu ya bima ya afya nchini.
Hayo yamebainishwa na Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Godbertha Kinyondo jijini Dar es Salaam leo Oktoba 25, 2022 amesema kuwa Katika Mwendelezo wa Chuo Kikuu Mzumbe Kusambaza matokeo ya Utafiti kwa wajasiriamali wadogo ambao ni Wajenzi, Baba Lishe, Mama Lishe, Wachuuzi pamoja na waendesha piki piki maarufu kama Bodaboda Wajenzi wadogo wadogo wameonekana kuwa hawana bima za afya.
Hawajajiunga na Mfuko wa Pensheni kwa asilimia 24.4 tu ndio waliohudhuria mafunzo rasmi lakini asilimia 75.6 hawana mafunzo rasmi na wengi wamesema kuwa wamepata mafunzo kutoka kwa Wajenzi wengine.
“Pia wengi wao wahawajajiunga na vikundi ambavyo vinawawezesha kuwasaidia katika mambo mengi hasa kupata bima za afya na Mfuko wa Pensheni kwa kuweza kuchangia shilingi 20,000 kwa mwezi na baada ya miaka kadhaa wakapata pensheni yao.” Amesema DKT. Kinyondo
Licha ya hayo Dkt. Kinyondo amewaomba waunde vingundi na Vikundi hivyo viwe na Uongozi bora, viwe na Katiba pamoja na Kuwa na malengo ili waweze kutimiza mahitaji ya wanankikundi kwa Ujumla.
“Katika kufanikisha hilo Chuo Kikuu Mzumbe tuko tayari kuwasaidia kurahisisha uundwaji wa vikundi hadi kufikia kutimiza malengo ya vikundi hivyo katika kuendeleza kazi zao.” Amesema
Kwa Upande wa Mtafiti Kutoka Chuo Kikuu Mzumbe, Aloyce Gervas amesema kuwa katika Uliofanywa na Chuo Kikuu Mzumbe umeonesha kuwa waajiliwa katika Sekta ya Ujenzi asilimia 67.8 hawana mikataba ya Kazi na hawazingatii Elimu ya Afya na Usalama mahali pa kazi.
"Kwahiyo hii inawafanya pale ambapo wanaendelea kufanya kazi katika majengo wanapopata changamoto mbalimbali za Kiafya inabidi mafundi wenyewe kujigharamia huduma za afya katika kutatua changamoto za kiafya zilizowakumba wakati walikuwa eneo rasmi la Kazi na kufanya kazi katika Majengo Makubwa." Amesema Gervas
Ametoa wito kwa wakandarasi na wanaotoa ajira kwa Mafundi Ujenzi wanapowaajiri mafundi katika kazi zao wazingatia zile kanuni na sheria za kazi.
"Kwamba hata kama anafanya kazi kwa muda mfupi ampe mkataba muda mfupi wa kazi anayoifanya ili kama ikitokea fundi amepata changamoto yeyote aweze kunufaika. Asitumie kipato chake kidogo alichokipata kwenye ile kazi kwa kwenda kijigharamia katika Matibabu.” Amesema
Pia Ametoa Wito kwa Mafundi kujiunga katika Vikundi kwani ni Asilimia 40.5 tu ndio wamejiunga kwenye vikundi pia amewaasa kuvirasimisha vikundi vyao, kuwa na katiba ili vikundi hivyo viweze kuwasaidia kupaza sauti kwenye maeneo yanayopata changamoto.
Kwa Upande wa Fundi Ujenzi kutoka Kikundi cha Sinza Construction, Maneno Juma Matanga amewashukuru Chuo Kikuu Mzumbe kwa kuwapa elimu juu ya Mifuko ya kijami na Bima ya Afya pia kuwapa ujasili wa kujinasibu kwa kazi wanayoifanya.
Amesema kuwa elimu wanayoipata imeweza kuwasaidia kutoka sehemu moja kwenda nyingine na kuondokana na mfumo wa kizamani.
"Malengo yetu sisi ni kufikia kila mwanachama wa Sinza Construction awe na bima ya Afya na pia tuwe tumejiunga na Mfuko wa hifadhi za jamii wa NSSF."
Kwa Upande wa fundi Ujenzi Mwanamke, Mwana Wete amesema kuwa Upande wa wanawake katika sekta ya Ujenzi kumekuwa na mwamko mdogo sana kwa sababu wanapitia changamoto nyingi hasa pale mtu anavyokuchukulia kwenye jamii na namna kazi hiyo inavyofanyika.
Pia amewashukuru Chuo Kikuu Mzumbe kwa kuwapa ushauri wa kujiunga kwenye vikundi pia amesema atawahamasisha wajenzi wengine waweze kujiunga katika vikundi ambavyo vitawawezesha kupata stahiki mbalimbali.
Licha ya hayo waliopo katika sekta ya ujenzi wameomba kupata mikopo endapo wakijiunga katika Vikundi vilivyosajiliwa na kuwa na Katiba.
Mhadhiri wa Chuo Kikuu Mzumbe, Dkt. Godbertha Kinyondo akizungumza na wajenzi wadogo wadogo jijini Dar es Salaam leo Oktoba 25, 2022 wakati akiwasilisha matokeo ya Utafiti uliofanyika kuanzia 2017 kwa afanyakazi wa sekta zisizo rasmi hapa nchini.
Mtafiti Kutoka Chuo Kikuu Mzumbe, Aloyce Gervas akizungmza na wajenzi leo jijini Dar es Salaam na kuwashauri kujiunga katika vikundi ili waweze kupata stahiki mbalimbali ikiwemo mikopo kutok serikalini.
Mmoja wa wajenzi akifafanua jambo wakati wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe wakiwasilisha matokeo ya Sekta ya ujenzi kujiunga na mfuko wa Kijamii na bima ya aftya.
Wajenzi wakisiliza wafanyakazi wa Chuo Kikuu Mzumbe jijini Dar es Salaam leo Oktoba 25, 2022 wakati akiwasilisha matokeo ya Utafiti uliofanyika kuanzia 2017 kwa afanyakazi wa sekta zisizo rasmi hapa nchini.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment