Wananchi wa Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro wametakiwa kutunza maji kitokana na upungufu wa maji kwenye mto Ruvu unaotoa Huduma za Majisafi katika Mikoa hiyo.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe. Amosi Makalla alipotembelea na kujua hali ya uzalishaji maji akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Dar es Salaam pamoja na Bodi ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA)
Makalla amesema kina cha majibhasa huku kwenye vyanzo vya uzalishaji wa maji kimeshuka kwa maana hiyo kutakuwa na upungufu wa maji kwa kiasi kikubwa kwa Mikoa hiyo.
"Tilitarajia mvua za mwezi wa Tisa na kumi kuwepo mvua za vuli ambazo zinakuja kusaidia kuongeza maji kwenye hivi vyanzo maji na pia kuna taarifa za Mamlaka ya Hali ya Hewa kuwa kitakuwepo na upungufu wa mvua na kuwepo kiangazi cha mda mrefu na ndo maana tumeshindwa kupata mvua za vuli.
Pia amesema kuwa Serikali pamoja na Bodi ya DAWASA kuna jitihada zimefanyika kwanza hiki kinachopatikanika kinatumika vizuri lakini pia kamati zote za kamati za ulinzi na usalama za mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro zimeweza kutimiza majukumu yake kwa wale wote wanaochepusha maji wanachukuliwa hatua ili kuweza kuongeza upatikani wa maji kwenye mto Ruvu.
"Hakuna kisingizio kingine chochote cha kina cha maji zaidi ya utegemezi wa mvua na hapa nasisitiza kuwa Serikali inafanya jitihada kwa hiki kidogo kilichopo kinawafikia wananchi na asije mtu akasema hata mvua inaweza kuletwa na Serikali." amesema Makalla
Pia Makalla amewataka DAWASA kumaliza kwa haraka mradi wa maji wa Kisarawe II uliopo Kigamboni ili kuweza kupunguza makali ya upatikanaji wa maji kwa wakazi wa Dar es Salaam pamoja na Pwani.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment