Mke wa Rais Mstaafu wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete na Mbunge wa Mchinga, Mhe Mama Salma Kikwete akiwasilisha mada kwenye kongamano la Taasisi ya Wanawake, wake wa Marais wa Afrika kwa Maendeleo (OAFLAD), alivutia washiriki kwa kuweza kuelezea mambo mengi na changamoto zinazomkumba mama na mtoto barani humo.
Pia aliwasilisha salamu za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na kusema Tanzania imepiga hatua kubwa katika masuala ya afya ya mama na mtoto, na sasa juhudi zinaelekezwa kwa vijana, na hivi karibuni, Tanzania imeanzisha mpango wa kuendelea kuwasomesha, watoto wa kike waliopata ujauzito wakiwa shuleni, wakati huko nyuma wanaopata uja uzito wakiwa shuleni, walifukuzwa shule.
Mama Salma Kikwete, aliwakaribisha wajumbe kutoka mataifa mengine ya Afrika kutembelea Tanzania ili kujifunza uzoefu na maendeleo ya Tanzania yaliyofikiwa nchini humo ili yaweze kutumika kama shamba darasa kwa nchi nyingine za Afrika na kuhimiza ushirikiano wa kimataifa katika kukuza afya na lishe ya wanawake, watoto wachanga, watoto na vijana.
Mhe Mama Salma Kikwete, ambaye alihutubia kongamano hilo kwa lugha adhimu ya Kiswahili, alipongeza mjadala wa mkutano huu, na kushauri maazimio ya kongamano hilo kutumika kwa nchi zote za Afrika kukabiliana na changamoto za lishe zinazowakabili bara la Afrika kufikia malengo ya SDGs katika nyanja za afya na lishe.
Taasisi ya Wanawake, wake wa Marais wa Afrika kwa Maendeleo (OAFLAD) ilianzishwa mwaka 2002, kwa wake wa Marais wa Afrika kuunda taasisi hiyo ya Wake wa Marais wa Afrika kwa lengo la kuwa na sauti ya pamoja, kusaidia wananchi wa bara la Afrika kwa wake hao kama wake wa Marais wa Afrika kutumia nguvu yao ya ushawishi na nafasi zao kama wake wa viongozi kusaidia huduma za afya na uwezeshaji wa wanawake na vijana. kwa kukusanya rasilimali na kuendeleza ushirikiano na wadau wote katika ngazi zote.
Mwisho.
Mke wa Rais Mstaafu wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, Mhe. Salma Kikwete (ambaye pia ni Mbunge wa Mchinga), akitembelea maonyesho ya wajasiliamali wa Burundi, wakati wa Kongamano la 3 la Viongozi Wanawake Barani Afrika, ambao ni wake wa marais, lililoandaliwa na Taasisi ya OAFLAD( The Organization of African First Ladies for Development) lililomalizika jijini Bujumbura Burundi hivi karibuni kujadili changamoto za afya na lishe kwa wanawake, watoto na vijana balehe.
Mke wa Rais Mstaafu wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mhe. Salma Kikwete (ambaye pia ni Mbunge wa Mchinga, akiwa na mwenyeji wake, Mama Angelina Ndayishimiye, mke wa Rais wa Burundi, Mhe. Evarist Ndayishimiye wakati wa Kongamano la 3 la Viongozi Wanawake Barani Afrika, ambao ni wake wa marais, lililoandaliwa na Taasisi ya OAFLAD( The Organization of African First Ladies for Development) lililomalizika jijini Bujumbura Burundi hivi karibuni kujadili changamoto za afya na lishe kwa wanawake, watoto na vijana balehe.
Mke wa Rais Mstaafu wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mhe. Salma Kikwete (ambaye pia ni Mbunge wa Mchinga), akiwapungia mkono wananchi wa Bujumbura, akiwa na mwenyeji wake, Mama Angelina Ndayashimiye, mke wa rais wa Burundi, Mhe. Evarist Ndayishimiye wakati wa Kongamano la 3 la Viongozi Wanawake Barani Afrika, ambao ni wake wa marais, lililoandaliwa na Taasisi ya OAFLAD( The Organization of African First Ladies for Development) lililomalizika jijini Bujumbura Burundi hivi karibuni kujadili changamoto za afya na lishe kwa wanawake, watoto na vijana balehe.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment