WAZIRI JAFO ATAKA UPANDAJI MITI UWE ENDELEVU KWA MANUFAA YA TAIFA LETU | Tarimo Blog

 

Na Mwandishi Wetu

WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)  Dkt.Selemani Jafo amesema ni vema suala laupandaji miti katika nchi yetu liwe endelevu ili kusaidia kuhifadhi mazingira.

Jafo aliyasema hayo baada ya kuongoza upandaji miti  uliofanyika katika Shule ya Msingi Mtoni wilayani Bagamoyo mkoani Pwani na kuratibiwa na benki ya Standard Chartered ambapo amewahimiza wananchi kuendelea kuhamasisha kupanda miti.

Ameongeza  upandaji wa miti kwa wingi kwenye mazingira ni njia moja wapo itakayosaidia kukabiliana na changamoto ya hewa ukaa inayoweza kuhatarisha maisha ya mwanadam.

Jafo ameipongeza Benki ya Standard Chartered kwa kunialika kuja kupanda miti kwenye shule hii naomba taasisi za serikali na binafsi nchini kuinga kwa mfano wa Benki ya Standard Chartered kuleta miche miti 1000 alisema Jafo.

 Aidha amesema ajenda ya mazingira ndiyo ajenda inayosababisha uchumi kuwa imara huku akiwataka wanafunzi kupeleka ujumbe kwa wazazi wao kushiriki katika zoezi zima la kupanda Miti katika maeneo yao.”amesema Jafo.

"Serikali imekuwa na mikakati mbalimbali katika kuhakikisha inatunza mazingira ili kuwa na mazingira safi miongooni mwa mikakati hiyo ni upandaji miti katika taasisi za serikali na binafsi nchini,"amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Herman Kasekende amesema amefarijika sana kuona watanzania wanapanda miti kwa wingi.
Nitaendelea kuunga mkono juhudi mbalimba na kuhakikisha Tanzania inakua ya kijani kama maelekezo ya serikari ya kupanda miti katika maeneo yote nchi nzima.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Dkt. Selemani Jafo,akihutubia wadau mbalimbali wa Mazingira wati wa upandaji miti 1000 iliyotolewa na Benki ya Standard Chartered iliyopandwa katika Shule ya Msingi Mtoni Wilaya ya
Bagamoyo Mkoa wa Pwani tarehe 22 Oktoba 2022.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Herman Kasekende akisoma hotuba yake wakati wa  upandaji miti 1000 iliyotolewa na Benki hiyo iliyopandwa katika Shule ya Msingi Mtoni Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani tarehe 22 Oktoba 2022 (PICHA ZOTE EMMANUEL MASSAKA WA MICHUZI TV) 



Wadau mabalimbali wa Mazingira wakimsiliza Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo (haupo pichani) 
    Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo  akipoka zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benkiya Standard Chartered, Herman Kasekende  kushoto ni Afisa Tawala Wilaya Magamoyo mkoa wa Pwani, Casilda Mgeni.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo  akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya  Wilaya ya  Bagamoyo Mkoa wa Pwani  tarehe 22 Oktoba 2022.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa katika picha ya patoja na viongozi wa CCM Wilaya Bagamoyo Mkoa wa Pwani jana tarehe 22 Oktoba 2022.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira), Mhe. Dkt. Selemani Jafo akiwa katika picha ya pamoja na uongozi wa Shule ya Msingi Mtoni Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani.




Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dk. Seleman Jaffo (katikati), akipanda mmoja ya miti 1000 iliyotolewa na Benki ya Standard Chartered iliyopandwa katika Shule ya Msingi Mtoni Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani na  (kushoto) ni  Afisa Tawala wa 
Wilaya Magamoyo, Casilda Mgeni, na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Herman Kasekende.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Standard Chartered, Herman Kasekende akipanda mti huku Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)  Dkt.Selemani Jafo akishuhidia katika Shule ya Msingi Mtoni Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani jana tarehe 22 Oktoba 2022.iliyotolewa na benki ya Standard Chartered.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)  Dkt.Selemani Jafo akishuhudia Viongozi wa CCM Wilaya Bagamoyo Mkoa wa Pwani wakipanda mti kwenye shule hiyo.
Sehemu ya Mti .(PICHA ZOTE EMMANUEL MASSAKA WA MICHUZI TV) 
 

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2