ANKAL MICHUZI AWAFUNDA MLIMANI TV | Tarimo Blog

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam 

Mwandishi wa Habari Mkongwe, Issa Michuzi ameendesha mafunzo ya uandaaji wa maudhui ya mtandaoni (Online Content Creation) kwa Waandishi wa Habari wa Mlimani TV, Mlimani Radio na The Hill Obsever.

Mafunzo hayo yametolewa leo Januari 30, 2023 katika ukumbi wa mikutano wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC), lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea uwezo waandishi hao ikiwa ni hatua madhubuti ya kuendana na kasi ya maendeleo ya teknolojia yanayojumuisha matumizi ya mitandao ya kijamii katika tasnia ya habari.

Akizungumza wakati akitoa mafunzo hayo, Bw. Michuzi amesema kuwa kufanikiwa kwa Mwandishi wa Habari maudhui ya mtandaoni kunategemea zaidi upekee wake, kujikita katika nyanja moja ya uandishi (Specialization) na kuzingatia hadhira yake anayoikusudia.

Awali akifungua mkutano huo Amidi wa Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC), Dkt. Mona Mwakalinga, amemshukuru Bw. Michuzi kwa kufika katika viunga vya SJMC na kutoa mafunzo kwa waandishi hao.

Kwa upande wao, viongozi, watangazaji na washiriki katika vituo hivyo vya habari wameonesha kuridhishwa na mafunzo hayo ambayo kwao wameona ni fursa pekee ya kujiendeleza kupitia mitandao ya kijamii.



 
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2