Mkurugenzi wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP) Lilian Liundi akizungumza wakati kufungua Mafunzo ya Bajeti yenye mrengo wa Kijinsia na Ushawishi kwa Wakuu wa Idara ya Mipango, Maafisa Utawi wa Jamii, Wakuu wa Idara ya maendeleo, maafisa Dawati la Jinsia, Maafisa maendeleo ya jamii Uwezeshaji kiuchumi, Maafisa Maendeleo wa Kata na Madiwani yaliyofanyika leo katika ukumbi wa TGNP jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya Washiriki katika mafunzo ya TGNP
Diwani wa Viti Maalum wa Jiji la Dar es Salaam Beatrice Nyamisango akitoa maelezo kuhusia ushiriki wa katika maamuzi kwenye bajeti inayolenga jinsia , jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya washiriki wa mafunzo ya Bajeti yenye mrengo wa jinsia na Mkurugenzi Mtendaji wa TGNP Lilian Liundo , jijini Dar es Salaam.Baadhi ya Washiriki katika mafunzo ya TGNP
*Yakutanisha baadhi ya wadau wakiwemo wanawake walioko katika maamuzi.
Na Chalila Kibuda,
MTANDAO wa Jinsia Tanzania (TGNP) umetaka wanawake walioko katika ngazi za maamuzi katika maeneo yao kuhakikisha wanaweka bajeti yenye mlengo wa kijinsia
Bajeti zikiwa katika fungu la pamoja ni changamoto kufatilia hivyo katika kurahisisha ufatiliaji huo bajeti ya inayotengwa kwa ajili ya jinsia.
Hayo yamesemwa Mkurugenzi wa TGNP Lilian Liundi wakati akifungua Mafunzo ya Bajeti yenye mrengo wa Kijinsia na Ushawishi kwa Wakuu wa Idara ya Mipango, Maafisa Utawi wa Jamii, Wakuu wa Idara ya maendeleo , maafisa Dawati la Jinsia, Maafisa maendeleo ya jamii Uwezeshaji kiuchumi, Maafisa Maendeleo wa Kata na Madiwani yaliyofanyika katika ukumbi wa TGNP jijini Dar es Salaam.
Amesema lengo la mafunzo hayo ni kuongeza uelewa juu ya umuhimu wa Upangaji wa bajeti, mipango na Sera zinazozingatia Jinsia miongoni mwa watoa maamuzi pamoja na kutambua mapengo yaliyopo kwenye eneo la ushawishi na kujenga uwezo wa stadi za utetezi kwa siku za zijazo kuweza kusimamia yale ambayo hayakuwa katika bajeti iliyopita.
Lilian amesema makundi yanayoshiriki wanaamini wako sehemu ya kufanya maamuzi ya kuhakikisha bajeti inayotoka katika maeneo yao ikizingaatia jinsia kutokana na uchambuzi mbalimbali unaofanywa katika Manispaa ,Miji pamoja na Halmashauri na wakati mwingie ngazi za vijiji.
Amesema katika Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025 (TDV 2025) imetambua kuwa mojawapo ya vichocheo vya ukuaji wa uchumi ni pamoja na jamii yenye muono wa kimaendeleo ambapo pamoja na mambo megine unakuwa na tamaduni wezeshi hususani kwa wanawake na makundi mengine kuangalia bajeti kama ina mrengo wa kijinsia.
Pia amesema haki za binadamu na za wanawake zinajadilwa kwa sababu wanawake hawajawa kwenye nafasi na fursa sawa kama ya wanaume kwani bado wananyanyaswa na kukandamizwa na kuonewa na mifumo ya maisha iliyopo hivyo wamekutana ili kubainisha changamoto zilizopo wakati wa upangaji wa bajeti yenye mrengo wa kijinsia.
“Mnakutana leo ili kupeana mrejesho kuhusu utekelezaji wa masuala muhimu tuliyokubaliana katika mafunzo yaliyofanyika Desemba ya mwaka 2022 kuhusuiana na Bajeti yenye mrengo wa kijinsia kwa Harmashauri ili kubainisha changamoto na mafanikio tuliyokutana nayo wakati wa utekelezaji wa kile tulichojifunza ikiwemo na kutengeneza mpango wa utekelezaji masuala muhimu tuliyokubaliana” alimesema Liundi
Diwani wa Viti Maalum wa Jiji la Dar es Salaam Beatrice Nyamisango amesema kuwa katika vikao amekuwa akitoa msisitizo suala kijinsia hata miundombinu.
Amesema kuwa katika bajeti wamekuwa wakiangalia lakini bado sana kwa wanawake kujitoa katika kupigania masuala ya jinsia hali ambayo inafanya wanaume kuweka vitu pamoja bila kuzingatia mahitaji ya jinsia.
Warsha hii imekutanisha washiriki kutoka Jiji la Dar es Salaam (Ilala) Halmashauri ya Kishapu mkoani Shinyanga , Manspaa ya Ubungo, Manispaa ya Kinondoni, Manispaa ya Temeke , Manispaa ya Kigamoni pamoja na Manispaa ya Kinondoni.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment