MMOMONYOKO WA MAADILI BAKWATA MWANZA YAOMBA ELIMU YA DINI IINGIZWE KWENYE MITAALA | Tarimo Blog


NA BALTAZAR MASHAKA, MWANZA

BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) Mkoa wa Mwanza,limeiomba
Serikali kuingiza somo la dini kwenye mitaala ya elimu kuwafanya watoto wawe na hofu ya Mungu katika kukabiliana na mmomonyoko wa maadili huku CCM ikipendekeza wanaolawiti wakatwe sehemu ya viungo vyao.

Pia BAKWATA imempongeza mfanyabiashara maarufu Kanda ya Ziwa na Mjumbe
wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (NEC)Mkoa wa Mara,Omari Christopher Gachuma kwa kuwakutanisha na kuwafuturisha waislamu kwa miaka 28 licha ya kuwa na imani tofauti ya dini.

Hayo yalielezwa jijini Mwanza,leo jioni kwa nyakati tofauti na viongozi
wa dini,Chama na Serikali wakati wa futari iliyoandaliwa na Gachuma kwa ajili
ya waumini wa dini ya Kiislamu kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhani.

Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza,Alhaji Hasani Kabeke,amesema viongozi wa dini na
jamii wanahangaika kusaka suluhu ya mmomonyko wa maadili ili kujenga nchi ya watu waadilifu, hivyo serikali iangalie namna ya kuingiza somo la dini kwenye mitaala watoto wasome elimu ya dini kwa kuwa hofu ya Mungu haipo..

“Tunahangaika na maadili kwa sababu mambo yameshaharibika,watoto
hawasomi elimu ya dinina na hawana hofu ya Mungu.Tumesikia matamko ya serikali kuhusu mmomonyoko wa maadili na vitendo vya ushoga na tunapoingeza kufuta vitabu vilivyoingiza mambo mabaya kwenye mitaala na kupiga marufuku watoto wa umri chini ya miaka 10 wasiingie shule za bweni,” amesema Sheikhe Kabeke.

Amesema vitendo vya ushoga serikali imeonyesha msimamo kupitia kwa Makamu
wa Rais Dk. Philipo Mpango huku Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiagiza vyombo vya dola viingie ndani kuchunguza na kudhihiti hilo na kuwataka waislamu kumwombea Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa suala la mmomonyoko wa maadili na chama kinachotawala.

Sheikhe huyo wa mkoa ametumia fursa hiyo kumpongeza Gachuma kwa kuwafururisha waislamu na wasio waislamu jijini Mwanza kwa miaka 28,anatoa mwangwi kwa wengine wenye uwezo na si kujionyesha bali liko ndani ya nafsi yake na amebeba mengi ya uislamu kwani kutoa ni moyo.

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Nyamagana, Peter Begga,amesema mmomonyoko wa maadili atalifikisha suala hilo juu ya Chama liingizwe kwenye ilani ya uchaguzi
iwe rahisi kutekelezwa na viongozi na kupendkeza watu wanaowalawiti watoto itungwe sheria ili kithibitika wakatwe kipande cha maumbile yao kupunguza ama ukomesha vitendo hivyo.

Kwa upande wake Mgeni rasmi katika futari hiyo,Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Hassan Masala kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza,Adam Malima,amesema Sheikhe Kabeke ana uhusiano mzuri na serikali,bila hivyo anaamini fursa nyingi wasingezipata na kuwataka waislamu kutunza na kudumisha amani huku akimshukuru Gachuma kwa upendo wa kuandaa na kushiriki ibada iliywakutanisha wengi na amekuwa mshiriki wa maendeleo ya mkoa,Chama na Serikali.

“Sheikhe Kabeke,mambo unayotendeka kwenye jamii Mwanza umeweza kusaidia
kuyatatua na hili la maadili kuna umuhimu wa kuhuisha mitaala yetu,kuna vitu
hatukufanya vizuri na ni wajibu wa serikali kuyaona na kuyaingiza yaliyo bora
kwenye mitaala ili kujenga kizazi cha maadili bora,”amesema Masala.

Naye Gachuma amesema anafarijika kuona waislamu wakiitikia mwaliko wake,anafahamu faida za uislamu ni nyingi na hivyo ataendelea kufuturisha hadi mwisho wa wa uhai wake duniani,pia uhusiano na marafiki zake wengi wakiwa waislamu kuliko wakristo,hana njia ya kutoka kwenye uhusiano huo na ataendelea kuyadumisha aliyoyaanzisha.

Mkuu wa Wilaya ya Rorya mkoani Mara, Juma Chikoka, amesema anayoyafanya
Gachuma kwa waislamu ni uwekezaji wa dhati katika mioyo ya watu kwani hawangalii miaka mingapi uliyoishi duniani bali ulifanya nini kilicho alama katika mioyo yao na kuahidi kuiga na kuiga si vibaya.

Akizungumzia mmomonyoko wa maadili,amewaasa waislamu na Watanzania
kuendelea kuheshimu mila,desturi na utamaduni wetu pia mataifa meingine yanayokumbatia hayo yaziheshimu mila zetu na kwamba wilayani Rorya amewatahadharisha atakayebainika kufanya vitendo hivyo sheria zipo zitachukua mkondo wake.
Sheikhe wa Mkoa wa Mwanza,Alhaji Hasani Kabeke,akizungumza na waumini wa dini ya Kiislamu (hawapo pichani) wakti wa futari iliyoandaliwa leo na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Mkoa wa Mara,Omari Christopher Gachuma,leo jijini humu.

Waumini wa dini ya Kiislamu, wakiwasikiliza baada ya viongozi wa dini, Chama na Serikali,baada ya kufuturu leo,futari iliyoandaliwa jijini Mwanza na Mjumbe wa NEC wa Mkoa wa Mara,Omari Christopher Gachuma.Picha zote na Baltazar Mashaka.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2