SERIKALI: USHOGA, USAGAJI, MAPENZI YA JINSIA MOJA HAYANA NAFASI TANZANIA ... TUNAPONGEZA MSIMAMO VIONGOZI WA DINI | Tarimo Blog


Na Mwandishi Wetu, Michuzi TV

SERIKALI ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk Samia Suluhu Hassan imewahakikishia Watanzania nchi yetu na kwamba Ushoga,Usagaji pamoja na mapenzi ya jinsia moja hayana nafasi.

Akizungumza katika viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam kwenye Tamasha la Msama lililoandaliwa maalum kwa ajili ya kuliombea Taifa pamoja na Rais Samia, Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Mhe. Nape Nnauye ametumia nafasi hiyo kutoa msimamo wa Serikali kuhusu ushoga, Usagaji na mapenzi ya jinsia moja kwa kueleza wazi hayana nafasi nchini.

Amesema kwamba nchi ya Tanzania haitapelekwa kwenye utamaduni wa kigeni vitabu vyote vya dini pamoja na Katiba yetu iko wazi juu ya haya ambayo viongozi wa dini mmyakemea. Kwa niaba ya Serikali nataka niwahakikishie Watanzania ushoga, ugagaji , mapenzi ya jinsi moja haya nafasi Tanzania.

"Wala hakuna sababu ya kumung'unya maneno msimamo wetu uko wazi Mungu amelibariki Taifa hili hatuwezi kufungua mlango wa laana, msimamo wa Rais yuko pamoja na viongozi wa dini wa nchi hii.Mmeonesha ujasiri wa wazi wazi kukemea haya ,Rais anawaungeni mkono na sisi wasaidizi wake tunawaungeni mkono ili Taifa letu liendelee salama,"amesema Waziri Nape aliyemwakilisha kwenye tamasha hilo ambalo limekwenda sambamba na nyimbo za muziki wa Injili za kumsifu na kumtukuza Mungu.

Awali wakati anaanza kuzungumza Waziri Nape amesema kwa niaba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan amempa kibali cha kufika kwenye tamasha hilo ambalo walimualika lakini kwa bahati mbaya ana majukumu mengine,hivyo amemuomba amuwakilishe.

"Sasa la kwanza nifikishe salamu za upendo kwenu, anawashukuru sana kwa kutenga muda wenu kila mmoja hapa anathamini muda wake alioutenga na kuja kushukuru Mungu kwa ajili ya nchi yetu na kwa ajili yake ,hivyo Mungu akubriki sana kwa muda wako,kwa maombi yako ,kwa moyo wako na uzalendo wako kwa nchi yetu,Rais anakushukuru sana sana

"Kwa kipekee nawashukuru viongozi wa dini wote kabisa,Maaskofu ,Mitume ,Manabii lakini kwa kipekee Alex Msama(muandaaji wa tamasha hili) na wenzako kwa kuandaa tamasha hili Mungu awabariki sana sana. Nikupitia shughuli kama hizi ndio nchi yetu inaenda mbele ,wanasiasa wanaweza wakapanga ya kwao lakini ninyi mlioitwa kwa jina lake mkisimama mkamuomba huyu Mungu tunayemuamini atatuonesha njia

"Salamu za pili za mheshimiwa Rais kwa muda na Serikali ya Awamu ya Sita tumewasikieni viongozi wa dini mkisema wazi wazi mnataka Taifa letu lisimamie nini kwenye maadili na utamaduni wetu ,tumewaeleweni vizuri na ndio msimamo wa Serikali kama ambavyo nimeeleza utamaduni wa kigeni hauna nafasi katika nchi yetu."
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Mhe. Nape Nnauye akizungumza jukwaani
Mchungaji na mwanzilishi wa Kanisa la Arise and shine Ministries Tanzania (Bulldozer) Boniface Mwamposa akishusha maombi kwa ajili ya kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye tamasha la pasaka lililofanyika katika viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na Mbunge wa Jimbo la Mtama, Mhe. Nape Nnauye akiserebuka jukwaani pamoja na muimbaji nyota wa nyimbo za Injili Upendo Nkone.
Muimbaji wa Nyimbo za Injili Jennifer Mgendi akiimba jukwaaani moja ya wimbo wake uitwao Moyo tulia









Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2