Njombe
JESHI la Polisi mkoani Njombe imewataka wazazi na walezi katika kipindi hiki cha sikukuu kujihakikishia usalama wa watoto wao pindi wanapoenda katika viunga mbalimbali kwani kwa sasa kumekuwa na unyanyasaji wa kingono kwa watoto na hasa wakiume na kupelekea watoto hao kuharibikiwa maumbile yao.
Kamanda wa Polisi mkoani wa Njombe Hamis Issah amesema watoto watakapotoka matembezini wazazi ama walezi wahakikishe wanawakagua ili kuhakikisha kuwa wapo salama.
"Sasa hivi kumekuwa na mfumuko wa unyanyasaji unaofanywa na watu wazima ama watoto wenyewe kwa wenyewe ambapo hujenga mahusiano ya jinsia moja kitu ambacho ni kinyume cha maadili"amesema Kamanda Issah
Kuhusu tukio la wanafunzi kadhaa katika moja ya shule ya sekondari mjini Njombe kutajwa kusimamishwa masomo kwa kukutwa na makosa mbali mbali ikiwemo mapenzi ya jinsia moja (Ushoga) amesema polisi wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo.
"Kuna taharuki kwenye mashule ya Sekondari vijana wamejihusisha na mapenzi ya jinsia moja lakini sahizi upelelezi unaendelea itakapokuwa tayari tutaeleza nini kimejiri,na nani amehusika"alisema Kamanda Issah
Aidha amesema jeshi hilo tayari limeimarisha ulinzi katika kipindi hiki cha sikukuu huku akiwataka madereva wa magari mbalimbali kuendesha magari yao kwa uangalifu bila uvunjifu wowote wa sheria ikiwemo kutokutumia kilevi kupilitiza.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment