WATAFITI, WABUNIFU WAOMBA USHIRIKIANO KWENYE UVUNAJI WA SUMU YA NYUKI | Tarimo Blog


Na Avila Kakingo, Michuzi Tv
WATAFITI pamoja na wabunifu wameitaka serikali kushirikiana nao ili kujua faida zinazopata kwenye ufugaji wa nyuki ikiwemo upatikanaji wa tiba wa magonjwa yasiyo yakuambikiza ambayo yanawaathiri wananchi kwa asilimia 73.

Akizungumza wakati wa kuwajengea uwezo waandishi wa habari jijini Dar es Machi 8, 2023 salaam kupitia Tume ya Sanyansi na Teknolojia COSTECH ili kuona umuhimu wa kuweza kuandika habari za kisayansi kwa weredi na umahiri, Mbunifu na Mtafiti wa mashine ya kuvunia sumu ya Nyuki, Patriki Kitosi aliesema kutokana na watanzania wengi kutokujua thamani na utajiri uliojificha kwenye ufugaji wa Nyuki imepelekea wafugaji wengi kukosa tija kwenye ufugaji na kujua mazao yake hasa Sumu.

Alifafanua kuhusiana na mashine mpya ambayo ameitengeneza ya kuvuna sumu ya nyuki Kitosi amesema inauwezo mkubwa wa kuvuna Sumu ya Nyuki bila kuwadhuru na kupelekea wafugaji kupata faida kubwa kutokana na soko zuri la sumu hiyo kwenye makampuni ya uzalishaji wa dawa za binadamu ikiwemo tiba ya Kansa na Magonjwa ya Moyo.

Aidha Kitosi aliongeza kuwa Nyuki wanauwezo wa kuzalisha mazao saba yenye thamani kubwa kama yatavunwa kwa utaalamu na ueledi kwa kutumia vifaa vya kisasa ikiwemo kifaa hicho cha kuvuna sumu ya Nyuki ambacho kitamsaidia mkulima kuvuna sumu hiyo ambayo inathamani kubwa ambapo uuzwa kwa Gramu mmoja inauzwa kwa Zaidi ya Shiling Laki moja na nusu (150,000) kwa nje ya nchi.

Kitosi alisema kupitia kifaa hicho kilicho tengenezwa hapa nchini kwa gharama nafuu chenye kutengeneza mtetemo au shoti kwa kutumia umeme kina uwezo wa kuwatia hasira na kupelekea kukishambulia na kuking'ata kifaa hicho kwa dakika thelathini suala ambalo urahisisha ukusanyaji wa sumu ya nyuki ambayo itaachwa na nyuki kwenye kifaa hicho baada ya kukingata na mfugaji kuifadhi kwenye kifaa maalum tayari kwa kuingiza sokoni kwa wenye viwanda vya utengenezaji wa dawa.

Mbunifu na Mtafiti wa mashine ya kuvunia sumu ya Nyuki, Patriki Kitosi akiwasilisha mada wakati wa kuwajengea uwezo waandishi wa habari jijini Dar es Machi 8, 2023 salaam kupitia Tume ya Sanyansi na Teknolojia COSTECH ili kuona umuhimu wa kuweza kuandika habari za kisayansi kwa weredi na umahiri


Katika hatua nyingine kitosia amesema nyuki wanakawaida ya kutofautiana kutoka bara moja mpaka bara jingine kutoka nchi moja na nchi nyingine ambapo amebanisha kuwa nyuki wenye uwezo wa kuzalisha sumu ambayo hutajika kwenye soko la uzalishaji dawa ni nyuki waliopo kwenye ukanda wa afrika kutokana na kuzalisha sumu yenye kemikali zinazo hitajika kutoka na misitu inayopatika Afrika kwa umaalum Tanzania.

Aidha aliomba serikali pamoja na wadau wamaendeleo kuweza kuwasaidia kwa kuwangozea uwezo kwa kuwaunganisha na taasisi za kifedha kutoa elimu kwa wafugaji kujua mbinu hizo hili waweze kufuga kwa tija kwa kuongeza kipato chao pamoja na kuongeza pato la taifa kupitia kodi baada ya kuuzwa kwa bidhaa hizo za mazao ya nyuki ambazo ndio marighafi muhimu katika kutengeneza dawa za magojwa ya sio yakuambukiza yanayoitesa jamii kwa asilimi zainazokadiriwa kufika 70.
Licha ya hayo Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS) walisema  kuwa binadamu kukang'atwa na mdudu nyuki kuna faida nyingi sana katika mwili wa binadamu ikiwemo ya kusaidia kuondoa sumu mwilini, hivyo kwa wale ambao watang'atwa hawana sababu ya kumuua nyuki.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2