Na Shukrani Kawogo, Njombe.
Mgombea wa ubunge jimbo la Ludewa Mkoani Njombe Joseph Kamonga ametangaza neema katika sekta ya kilimo, barabara, uvuvi pamoja na mradi wa linganga na mchuchuma.
Neema hiyo ameitoa wakati wa uzinduzi wa kampeni uliofanyika katika kata ya mlangali jimboni humo na kusema kuwa atahakikishia wananchi wa liganga na mchuchuma wanalipwa fidia na kuyafanya maeneo hayo kuwa huru.
Aidha aliongeza kuwa katika sekta ya uvuvi ataboresha vitendea kazi kuwa vya kisasa zaidi pamoja na kuanzisha miradi ya ufugaji samaki.
Hata hivyo kwa upaande wa wakulima amesema ataweka mkazo katika kilimo cha mazao ya kimkakati ili kiwe chenye tija na kuweza kupata masoko mazuri.
Uzinduzi huo ulihudhuliwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho mkoa , wilaya na wagombea udiwani wa CCM kutoka katika kata mbalimbali.

Katibu wa CCM wilaya Bakari Mfaume akiwatambulisha wagombea udiwani kutoka kata 26 katika uzinduzi wa kampeni wa Jimbo la Ludewa
Kikundi Cha ngoma ya Mganda kutoka kata ya Lupingu wakitumbuiza katika uzinduzi wa kampeni katika Jimbo la Ludewa mkoani Njombe.
Aliyekuwa mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Ngalawa (kulia ) akimnadi mgombea ubunge wa Sasa Joseph Kamonga katika uzinduzi wa kampeni
Mama mzazi wa ugombea ubunge jimbo la Ludewa CCM Joseph Kamonga akiwa amepiga magoti kuwashukuru Wana CCM kwa kumpa ridhaa mtoto wake kuipeperusha bendera ya Chama hicho huku akimuombea kura kwa wananchi za kumpitisha kuwa mbunge.
Msanii wa muziki wa kizazi kipya anayefahamika kwa jina la The Cute, akitumbuiza jukwaani katika uzinduzi wa kampeni katika Jimbo la Ludewa huku Wanacha wa CCM akiwemo mgombea ubunge wa jimbo hilo Joseph Kamonga wakionekana kwenda naye sambamba
Mgombea ubunge jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akionesha ilani ya Chama Cha mapinduzi 2020/2025 kwa wananchi waliohudhuria uzinduzi wa kampeni jimboni humo
Mwenyekiti wa vijana CCM wilaya ya Ludewa Theopista Mhagama ( kushoto) akitumbuiza pamoja na katibu mwenezi wa mkoa wa Njombe Erasto Ngole
Msanii wa muziki wa kizazi kipya Beka Flavor akitumbuiza kwenye uzinduzi wa kampeni katika jimbo la Ludewa mkoani Njombe
Mgombea ubunge Jimbo la Ludewa Joseph Kamonga akimtambulisha mke wake katika uzinduzi wa kampeni
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment