STAMICO KUIMARISHA UCHUMI WA KYERYWA | Tarimo Blog

SHIRIKA la Madini la Taifa (STAMICO) lafufua uchumi wa wachimbaji wadogo wa kyerwa kwa kuwaletea soko la uhakika la madini bati kwa kuanza kununua madini hayo kutoka kwa wachimbaji wadogo ili kuinua hali ya uchumi.

Ununuzi huo umeanza mara baada ya kufungua tena biashara ya madini katika mnada wa kwanza uliofanyika katika soko la madini kijiji cha Nyaruzumbura wilaya ya Kyerwa na kushuhudiwa na Mkuu wa wilaya ya Kyerwa Mhe. Rashid Mwaimu mapema wiki hii.

C:\Users\USER\Desktop\kyerwa\_MG_0300.JPG

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO (katikati) akiweka madini katika kifaa cha kuhifadhia madini ya bati baada kupokea kwa mchimbaji mdogo na kushuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mh. Rashid Mwaimu (wa kwanza kulia) mara baada ya ufunguzi wa kununua madini ya bati


Akiongea wakati wa kufungua ununuzi huo Kaimu Mkurugenzi wa STAMICO Dkt Venance Mwasse amesema STAMICO imeamua kuwa mnunuzi wa madini bati ili kuwakomboa wachimbaji ambao wamekuwa wakinyanyasika wakati wa kuuza madini yao kutokana na kukosa mbadala wa mnunuzi. 

“Tumeamua kununua madini haya ili kuwapatia soko la uhakika litakalowafanya wachimbaji warudi migodini kuendelea na uchimbaji, kwa kutoa bei shindani katika soko itakayowaongezea kipato na kuwasaidia kuinua uchumi wa Kyerwa”alisisitiza Dkt.
Mwasse.

Amesema katika kutekeleza jukumu lake la kumlea na kumsimamia mchimbaji mdogo STAMICO imejipanga vizuri kuhakikisha biashara hii inakuwa endelevu, ya uwazi yenye kuleta tija kwa mchimbaji kwa kuweka bei inayojumuisha gharama za maduhuri ya serikali na inayoendana na soko la dunia. 


Akishuhudia STAMICO ikipokea sheheni ya madini ya bati kutoka kwa wachimbaji wadogo; Mkuu wa Wilaya ya Kyerwa Mhe. Rashid Mwaimu amesema, STAMICO imekuwa mkombozi wa wachimbaji wadogo ambao kwa siku nyingi walikuwa katika dimbwi kubwa la umasikini lililosabishwa na kukosekana kwa soko la madini lenye ushindani. 

C:\Users\USER\Desktop\kyerwa\_MG_0286.JPG

Mkuu wa wilaya ya kerwa akifuraia makabidhiani ya madini ya bati yaliyofanyika kati ya STAMICO na wachimbaji wadogo baada ya kufungua ununuzi wa madini ya bati.

Amefurahishwa kuona STAMICO imechukua jitihada za haraka katika kutatua changamoto ya soko la madini na kuhakikisha biashara ya madini inarudi, jambo litakalochochea kukua kwa uchumi wa wachimbaji wa Kyerwa.

C:\Users\USER\Desktop\kyerwa\_MG_0306.JPG

Kaimu Mkurugezi Mtendaji wa STAMICO Dkt Venance Mwasse (katikati) akitoa maelezo jinsi biashara ya madini itakayoendeshwa na kuwashukuru wachimbaji wadogo mara baada ya kupokea madini

 “STAMICO imekuja na kifurushi cha utatuzi wa soko la madini ya bati ili kuhakisha soko linarudi katika hali yake kwa nguvu kubwa, soko leo ni kama tunalifungua upya tena kwa nguvu mpya, kasi mpya, hali mpya na kuhakikisha uchumi wa Kyerwa unang’ara, ule mdororo wa kiuchumi unaondoka” alisisitiza Mhe. Mwaimu

Amewataka wachimbaji wadogo kuongeza uzalishaji na kuongeza thamani ya madini yao ili kuhakikisha wanazalisha madini yatakayouzwa kwa bei ya juu ili kujiongezea kipato kitakacho boresha hali za maisha na kuondoa mdororo wa kiuchumi.

Wakati huo huo Afisa Madini Mkazi wa Mkoa Kagera Mha. Lucas Mlekwa amewataka wachimbaji wadogo kuuza madini yenye sifa stahiki zinazokubalika kimataifa, kwa kuwa STAMICO kama wanunuzi wangine wamekuja na utaratibu wa biashara unaofuata mfumo wa bei na viwango vya madini ya bati vya soko la kimataifa ili kufanya biashara endelevu yenye kuleta sifa na kuongeza pato la Taifa.

Kurejeshwa kwa biashara ya madini wilayani Kyerwa kumewarudisha tena wachimbaji wadogo mgodini ambao walikuwa wamezipa mgongo shughuli za uchimbaji na hapa walikuwa na machache ya kusema baada ya ufunguzi.

Akiongea kwa upande wa wachimbaji wadogo bw. Kiongozi wa shirikisho la wachimbaji wadogo Karagwe (KAREMA) ameiomba STAMICO kuendelea kununua madini hayo kadili wachimbaji watakavyoleta sokoni na kuangalia namna ya kutatua changamoto za vitendea kazi.

Bw. Jackson John Afisa Mtendaji wa kijiji cha Nyaruzumbura amesema STAMICO imeleta nuru kwa wananchi wake ambao walikuwa wanakosa mnunuzi wa madini wanaochimba jambo lilichochea hali ngumu ya uchumi.

 STAMICO imeanza kununua madini ya bati kutoka kwa wachimbaji wadogo ili kuwakomboa wachimbaji kwa kuleta ushindani katika soko ili kutatua tatizo la soko la madini lililokuwa likilalamikiwa kwa muda mrefu.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2