MHANDISI EVARIST NDIKILO AHIMIZA UWEKEZAJI BONDE LA UMWAGILIAJI RUVU | Tarimo Blog

 

Uwekezaji wa teknolojia ya kisasa utachangia uzalishaji wa mazao ya kutosha na kukuza uchumi wa kipato kwa wakulima wa bonde la umwagiliaji la Ruvu wilayani Bagamoyo. Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo alipokuwa akizungumza na wanachama wa Chama cha Wakulima wa Umwagiliaji katika bonde la Ruvu (CHAURU) Jumamosi  ya tarehe 10 Oktoba .

Mhandisi Ndikilo akitembelea maeneo mbalimbali ya kilimo cha mpunga, korosho na nanasi katika bonde hilo amefurahishwa na jitihada za wakulima wadogo wadogo za kutaka kujikwamua na umasikini wa kipato na kuwaomba wadau mbalimbali wenye uwezo wa kifedha kuwasaidia kwa kuwekeza katika kilimo cha kisasa zaidi, na hasa matumizi ya zana na pembejeo  bora za kilimo.

Amesisitiza kuwa serikali itakuwa bega kwa bega na chama hicho ili kuhakikisha kuwa changamoto mbalimbali zinazowakabili zinatafutiwa ufumbuzi kwa haraka. Ameiagiza serikali ya wilaya kwa kushirikiana na tarura kuboresha miundombinu ya barabara  ili zipitike mwaka mzima lengo likiwa ni kurahisisha ubebaji wa mazao na zana za kilimo.

Ili kuboresha miundombinu ya umwagiliaji Mkuu wa Mkoa amesema ameshawasiliana na ubalozi wa China na wao wameahidi kuwa wako tayari kufanya ukarabati. I kumbukwe kuwa serikali ya China ndiyo ilijenga miundombinu ya umwagiliaji wa bonde la Ruvu.

CHAURU ilikuwa ikiadhimisha miaka 18 tangu kuanzishwa kwa ushirika wa wakulima wa umwagiliaji katika bonde la mpunga la Ruvu. Maadhimisho hayo yaliyofanyika kwa siku tatu yameendana na maonesho ya bidhaa na zana za kilimo kutoka kwa wadau mbalimbali.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akitoa hotuba yake kwa viongozi na Wanachama wa chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu(CHAURU) waliofika kumsikiliza wakati wa kufunga maadhimisho ya pili ya siku ya CHAURU yaliyoendana na maonesho ya Bidhaa za kilimo pamoja na mazao ya kilimo hicho kinachofanyika katika ushirika huo.
Mwenyekiti wa Bodi wa Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu(CHAURU) Sadala Chacha kizungumza kuhusu historia ya ushirika huo ulioanzishwa mwaka 2002 pamoja na changamoto wanazozipata ndani na nje ya ushirika huo wakati wakati wa kufunga maadhimisho ya pili ya siku ya CHAURU yaliyoendana na maonesho ya Bidhaa za kilimo pamoja na mazao ya kilimo hicho kinachofanyika katika ushirika huo.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo, viongozi wa CHAURU, pamoja na wadau wa kilimo wakishuhudia uvunaji wa mpunga katika moja ya shamba lililopo kwenye eneo la CHAURU wakati wa maadhimisho ya siku tatu ya Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu(CHAURU).
Uvunaji wa mpunga ukiendelea
Baadhi ya mashamba ya mpunga yaliyopo katika eneo la CHAURU
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akiangalia mpunga mara baada ya kutolewa shambani alipotembelea mashamba ya mpunga katika eneo la CHAURU  wakati wa kilele cha maadhimisho ya pili ya siku ya Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu(CHAURU) itakayoedana na maonesho ya siku tatu kuanzia leo tarehe 08 hadi tarehe 10 Oktoba mwaka 2020
Muonekano wa mpunga mara baada ya kuvunwa kwenye moja ya shamba lililopo katika eneo la CHAURU
Mwenyekiti wa Bodi wa Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu(CHAURU) Sadala Chacha akitolea ufafanuzi Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kuhusu maji yanayotumika kwenye shughuri za kilimo cha umwagiliaji katika shamba la CHAURU. Mkuu wa mkoa huyo ametembela shamba hilo ili kujionea shughuri mbalimbali za kilimo zinazofanyika katika shamba hilo.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akiangalia mchele mara baada ya kukobolewa kwenye kinu kilichopo katika eneo la CHAURU wakati alipokuwa anatembelea na kujionea shughuli zinazofanyika katika eneo hilo wakati wa kilele cha maadhimisho ya pili ya siku ya Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu(CHAURU)
Baadhi ya magunia ya mpunga yalitayari kukobolewa kwenye kinu hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akikagua shamba la nanasi lililopokatika eneo la chamba la CHAURU wakati wa kutembelea shamba hilo na kujionea shughuri zinazofanyika katika eneo hilo wakati wa kilele cha maadhimisho ya pili ya siku ya Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu(CHAURU)
Meneja Ufundi wa Agricom Africa Ltd,  Philipo William akitoa ufafanuzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kuhusu kampuni hiyo inavyowakopesha na kutoa mikopo ya vifaa vya kilimo vya kisasa kwa wakulima ili kuweza kufikia malengo waliyojiwekea wakati wa kilele cha maadhimisho ya pili ya siku ya Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu (CHAURU) itakayoendana na maonesho ya siku tatu kuanzia leo tarehe 08 hadi tarehe 10 Oktoba mwaka 2020
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akikagua baadhi ya bidhaa za Agricom Africa Ltd alipokuwa anatembelea mabanda ya wakulima pamoja na wadau wa kilimo wakati wa wakati wa kufunga maonesho ya siku tatu kuanzia  tarehe 08 hadi tarehe 10 Oktoba mwaka 2020 ikiwa ni maadhimisho ya miaka 18 ya kuanzishwa kwa Ushirika huo Chalinze mkoani Pwani.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akiangalia moja na bidhaa inayotumika kurutubisha ardhi alipokuwa  anatembelea mabanda ya wakulima pamoja na wadau wa kilimo wakati wa wakati wa kufunga maonesho ya siku tatu kuanzia  tarehe 08 hadi tarehe 10 Oktoba mwaka 2020
Mwenyekiti wa The winners group,  Winjuka Mashenene akifafanua kuhusu namna walivyojipanga kama vijana kuwekeza kweneye kilimo kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo alipokuwa anatembelea baadhi ya mabanda mbalimbali wakati wa kufunga maonesho ya siku tatu kuanzia  tarehe 08 hadi tarehe 10 Oktoba mwaka 2020 ikiwa ni maadhimisho ya miaka 18 ya kuanzishwa kwa Ushirika huo Chalinze mkoani Pwani.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akimsikiliza Mratibu wa usambazaji wa teknolojia na mahusiano TARI-Dakawa, Fabiola Langa apokuwa anatolea ufafanuzi kuhusu mbegu mbalimbali za mpunga zinazoweza kuinua kilimo na namna ya mkulima kuzitumia mbegu hizo wakati wa kufunga maonesho ya siku tatu kuanzia  tarehe 08 hadi tarehe 10 Oktoba mwaka 2020 ikiwa ni maadhimisho ya miaka 18 ya kuanzishwa kwa Ushirika huo Chalinze mkoani Pwani.
Meneja wa chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu (CHAURU) Victoria Olotu  akitolea ufafanuzi kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo kuhusu mchele  pamoja na Korosho zinazolimwa katika  hilo alipokuwa anatembelea baadhi ya mabanda mbalimbali kwenye maonesho yatakayofanyika kwa siku tatu kuanzia tarehe 08 hadi tarehe 10 Oktoba, 2020.
Baadhi ya Wanachama wa chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu (CHAURU) pamoja na wananchi wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo wakati wa ufungaji wa wa maadhimisho ya pili ya siku ya CHAURU yaliyoanza taehe 08 hadi leo taehe Oktoba 10, 2010.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo  akitoa zawadi kwa wadau mbalimbali wa kilimo wa wakati wa ufungaji wa wa maadhimisho ya pili ya siku ya CHAURU yaliyoanza taehe 08 hadi leo taehe Oktoba 10, 2010.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo  tuzo ya shukrani kutoka kwa uongozi wa chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu (CHAURU) wa wakati wa ufungaji wa maadhimisho ya pili ya siku ya CHAURU yaliyoanza taehe 08 hadi leo taehe Oktoba 10, 2010.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo  akionesha tuzo ya shukrani aliyopewa na uongozi wa CHAURU kwa kuweza kuwahamasiha kulia kilimo cha kisasa ili kufikia malengo waliyojiwekea kama ushirika wakati wa ufungaji wa wa maadhimisho ya pili ya siku ya CHAURU yaliyoanza taehe 08 hadi leo taehe Oktoba 10, 2010.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo  akipokea zawadi mbalimbali kutoka kwa wakulima wa chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu(CHAURU) wa wakati wa ufungaji wa wa maadhimisho ya pili ya siku ya CHAURU yaliyoanza taehe 08 hadi leo taehe Oktoba 10, 2010.

Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akiwa kwenye picha za pamoja na viongozi, wanachama na wadau wa kilimo wakati wa kufunga maadhimisho ya siku tatu ya Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu(CHAURU).

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2