Katika kuadhimisha miaka 18 ya Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu(CHAURU), Taasisi ya Utafiti Tanzani( TARI) imeshiriki katika maonyesho ya kilimo yaliyofanyika viwanja vya ofisi ya CHAURU kuanzia tarehe 8 hadi tarehe Oktoba 10, 2020
Akizungumza kwenye maonesho hayo Mratibu wa usambazaji wa teknolojia na mahusiano TARI-Dakawa, Fabiola Langa amesema wakulima wa CHAURU wamekua wakinufaika na Teknolojia za TARI zikiwepo matumizi ya mbegu Bora hasa katika zao la mpunga. Wakulima wa Ushirika wa CHAURU wamekua wakitumia mbegu ya mpunga aina ya TXD306 (SARO 5) ambayo wamekua wakiipata kutoka Taasisi ya Utafiti Tanzania (TARI).
Katika maadhimisho ya siku tatu ya Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu(CHAURU) TARI imeonyesha mbegu Bora mbambali za mpunga zikiwemo mbegu mbili mpya ikiwemo TARI RIC 1 ambayo inanukia kama supa na ina mavuno mengi pamoja na TARI RIC 2 ambayo ina mavuno mengi na kustahimili ukame na magonjwa. Hata hivyo walitoa mafunzo juu ya mbegu za mpunga aina ya SATO 1 na SATO 9 ambazo zina uwezo wa kustahimili mashamba ambayo yameathiriwa na Magadi chumvi.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akimsikiliza Mratibu wa usambazaji wa teknolojia na mahusiano TARI-Dakawa, Fabiola Langa apokuwa anatolea ufafanuzi kuhusu mbegu mbalimbali za mpunga zinazoweza kuinua kilimo na namna ya mkulima kuzitumia mbegu hizo wakati wa kufunga maonesho ya siku tatu kuanzia tarehe 08 hadi tarehe 10 Oktoba mwaka 2020 ikiwa ni maadhimisho ya miaka 18 ya kuanzishwa kwa Ushirika huo Chalinze mkoani Pwani. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi wa Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu(CHAURU) Sadala Chacha
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akitazama moja ya mbegu Bora za TARI alipotembelea banda hilo wakati wa maonesho ya ya siku tatu ya wakulima wa CHAURU pamoja na wadau wa kilimo ikiwa ni maadhimisho ya miaka 18 ya kuanzishwa kwa Ushirika huo Chalinze mkoani Pwani. Wa kwanza kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi wa Chama cha Ushirika wa Wakulima wa Umwagiliaji Ruvu(CHAURU) Sadala Chacha
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment