Na Lusajo Frank DSJ
JOTO la uso wa dunia kwa mwezi uliopita wa Septemba, 2020 lilikuwa katika kiwango cha juu zaidi kuwahi kurikodiwa kwa mwezi huo.
Viwango vya joto kuanzia mwezi Januari ni vya juu zaidi tangu mwaka 2016, ambao ndio mwaka wenye joto la juu tangu vipimo vya joto vilipoanza kurikodiwa.
Hayo ni kwa mujibu wa mpango wa Umoja wa Ulaya wa kuchunguza joto la dunia "Copernicus Climate Change".
"Copernicus Climate Change" umesema miezi mitatu ya mwaka huu, Januari, Mei na Septemba ilivunja rekodi ya joto kuliko miezi kama hiyo ya miaka iliyotangulia, huku Juni na Aprili zikiwa sambamba na rekodi iliyopo kwa miezi hiyo.
Mwanasayansi wa mpango huo, Freja Vambourg ameliambia shirika la habari la AFP kuwa tofauti ya viwango vya joto vya mwaka 2016 na mwaka 2020 ni ndogo sana.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment