STARTIMES YAADHIMISHA WIKI YA HUDUMA KWA WATEJA DAR | Tarimo Blog

 
Mkuu wa kitengo huduma kwa wateja Gaspa Ngowi akizungumza na waandishi wahabari jijini Dar es salaam katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa wateja.
Mkuu wa kitengo cha Mawasiliano wa kampuni ya startimes Deusdedith Manugulilo akitoa taarifa juu ya maboresho ya kitengo hicho ili kuwafikia wateja kwa urahisi kupitia simu ya mkononi pamoja na mitandao ya kijamii.
Baadhi ya wateja waliofika kupata huduma katika wiki ya maadhimisho kwa wateja wakiwa pamoja na wafanyakazi wa kampuni ya startimes jijini Dar es salaam wakikata keki pamoja.
keki maalum iliyoandaliwa na kampuni ya startimes katika wiki ya maadhimisho kwa wateja.

Husein juma ni mmoja ya mteja aliefika dukani na kupatiwa baadhi ya taarifa ya jinsi ya kujiunga na king'amuzi cha startimes katika maadhimisho ya wiki ya huduma kwa watejea.

KAMPUNI  ya startimes limited yaadhimisha  wiki ya huduma kwa wateja kwa kukata keki pamoja na wateja wao.

Akizungumza na waandishi wahabari jijini Dar es salaam, wakati wa kuadhimisha wiki hiyo Mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja Gaspa Ngowi  amesema kila mwaka mwanzoni mwa mwezi octoba kila kampuni,taasisi pamoja na mashirika yanaadhimisha wiki ya huduma kwa wateja .

" Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja ,sisi startimes tunawahaidi wateja wetu wote kwamba tupo nanyi bega kwa bega kuhakikisha mnapata huduma zilizo Bora,nafuu na kwa wakati sahih."

Kwa upande wake Meneja wa kitengo cha mawasiliano wa kampuni ya startimes Deusdedith Manugulilo amesema kitengo hicho Cha mawasiliano kitaendelea kuboresha zaidi huduma hizo pindi mteja atakapopiga simu nakuhitaji marekebisho yoyote yale kwenge king'amuzi chake.

"Tuna wafanyakazi wakutosha hivyo ni wape tu rai wateja kupiga simu ili kupata taarifa pale ambapo watapata ukakasi kujua huduma zetu kwa ujumla.


Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2