Na Pamela Mollel Michuzi TV,ARUSHA
Zaidi ya Taasisi kumi zinazojishughulisha na shughuli za uhifadhi zimekutana Wilayani Monduli Mkoani Arusha ikiwa ni kutafuta maoni ya namna ya kufanya uhifadhi endelevu pamoja na kuondoa migogoro inayojitokeza katika baadhi ya vijiji vinavyozunguka hifadhi
Pia Ongezeko la mifugo,mimea vamizi,muingiliano kati ya wanyamapori mifugo na binadamu ni miongini tu mwa changamoto zinazotajwa katika uhifadhi,
Meneja Uhifadhi kutoka Shirika la Nature Conservancy Arusha
alisema kuwa wao pamoja na wataalam wa uhifadhi wamekuwa wakikusanya maoni ya nini kifanyike kuielimisha jamii juu ya umuhimu wa uhifadhi
Taasisi ya Randlen WMA inawakutanisha Wadau wa uhifadhi kutoka taasisi mbambali ikiwa ni kukukusanya maoni ya nini kifanyike katika miaka mitano ijayo 2021-2025 hususani katika vijiji vinavyozunguka hifadhi ili kuweka mahusiano mazuri baina ya vijiji na uhifadhi
Meneja Randlen WMA Meshurie Melembuke alisema kuwa kabla ya wao kukutana mchakato ulianzia chini kule vijijini kwa kukutana na Halmashauri za vijijini na baadhi ya wanajamii ambao ni Vijana,Wazee ,Wazee wakimila na wawakilishi wa WMA ili kukusanya maoni
Aidha Melembuke alisema kuwa kukutana kwao itasaidia kutengeneza dira ambayo inaendana na malengo ya Taifa ifikapo 2025 na kwa kufanya hivyo wanaamini itasaidia wasonge mbele na rasilimali fedha watajua waelekeze wapi kwa vipaumbele
Mkuu wa Wilaya ya Monduli Edward Balele akifungua Warsha ya siku moja iliyofanyika katika eneo la Mto wa Mbu Wilayni Monduli aliweka msisitozo mkubwa ni kwa namna gani taasisis za uhifadhi zinayaangalia maeneo yenye wanyama ambayo yametelekezwa kwa mda mrefu.
"Maeneo haya yapo yametelekezwa kwa mda mrefu na yalikuwa maeneo mazuri tukiyaangalia maeno haya vizuri itasaidia hata changamoto ya wanyama kugongwa itapungua kwa kuwa hata kama watavuka barabara kwaajili ya kutafuta maji hawatavuka tena kwakuwa maeneo hayo yameboreshwa"alisema Balele
Zoezi hili limeshirikisha taasisis mbalimbali ikiwa ni kuangalia nini kifanyike kuboresha uhifadhi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Monduli Steven Ulaya akizungumza katika warsha hiyo
Wadau wa uhifadhi wakifatikia warsha
Meneja uhifadhi kutoka Shirika la Nature Conservancy Arusha Alphonce Mallya akizungumza katika warsha hiyo
Meneja wa Taasisi ya Randlen WMA Meshurie Melembuke akizungumza katika warsha hiyo ya siku moja
Mkuu wa Wilaya ya Monduli Edward Balele akifungua warsha ya siku moja iliyofanyika katika eneo la mto wa Mbu Wilayani Monduli iliyowakutanisha wadau wa uhifadhi kutafuta maoni ya namna ya kufanya uhifadhi endelevu.
Wadau wa uhifadhi wakifatilia warsha
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment