Na Mwamvua Mwinyi, CHALINZE
MBUNGE wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete amewahakikishia
wananchi wa Kata ya Pera na Chalinze kuwa Serikali itaendelea kutatua
kero za migogoro ya Ardhi katika Halmashauri hiyo .
Akizungumza na wananchi wa Kata ya Pera, amewahakikishia wananchi kuwa wamejipanga vizuri kumaliza kero za mipaka hasa ile isiyokwisha kati
ya Kitongoji cha Pingo na Chamakweza ambao umedumu kwa takribani
miongo Miwili.
Awali akiwa katika Kitongoji cha Pingo, Mbunge aliweza kufanya mkutano
wa wazi na Wananchi ambapo pia aliongozana na watalaam mbalimbali wa
Idara pamoja na viongozi wa ngazi ya Vitongoji, Kata na Wilaya
wakiwemo Wanasiasa.
Mbunge amewaahidi Wananchi hao kuendelea kutoa ushirikiano huku
akiwashukuru kwa kukichagua Chama Cha Mapinduzi CCM ikiwemo kumpatia
asilimia zaidi ya 94 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli.
Katika mkutano huo ambao Mbunge alipokea pia kero mbalimbali
zinazowakabili Wananchi ikiwemo migogoro ya mipaka,
Mgogoro ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji, Fursa za TASAF, mikopo
ya Jamii, Afya na mengineyo.
Hata hivyo Mbunge aliweza kutolea ufafanuzi baadhi ya kero za Wananchi
ambazo zimeanza kufanyiwa kazi na kuwakumbusha kuwa serikali haikuwa
imelala ilikuwa inafanya kazi, huku zingine akiahidi kuzichukua kwa
ajili ya kuzitafutia ufumbuzi.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment