*Samwix kufuta leseni kwa makosa ya mara kwa mara
Na Chalila Kibuda, Michuzi TV
JESHI la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani kimesema madereva wasiofuata sheria halitawavumilia pamoja na kuwepo kwa opereshani mara kwa mara
Oparesheni katika kituo cha Ubungo ilihusisha Mamlaka ya Usafiri Barabarani (LATRA) Mabalozi wa Usalama Barabani (RSA) pamoja na Jeshi la Polisi kikosi cha Usalama Barabarani kikiongozwa Kamanda wa Kikosi hicho Wilbroad Mutafungwa.
Oparesheni hiyo ilikwenda kwa Ukaguzi wa Mabasi, Kuangalia nauli zilizowekwa zinaendana na tiketi za kampuni za mabasi.
Akizungumza katika Oparesheni na utoaji wa elimu Kamanda wa Polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani Wilbroad Mutafungwa wakati alipokuwa katika katika oparesheni na utoaji wa elimu kwa madereva wa Mabasi katika kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.
Kamanda Mutafungwa amesema kuwa nchi iko katika amani hivyo asitokee mtu akasababisha watu wengine wasiwe na amani kwa kusababisha ajali zinazotokana uzembe.
Aidha amesema kuwa wataendelea na oparesheni kwa nchi nzima pamoja uimarishaji wa taa za barabarani kwa madereva wasiofuata sheria za usalama Barabarani.
Nae Mkuu wa kituo cha Ukaguzi wa Mabasi katika kituo Mabasi Ubungo Ibrahim Samwix amesema kuwa dereva yeyote atakayefanya makosa yanayojirudia watanyang'anywa leseni zao.
Amesema kuwa madereva wanatakiwa kufuata sheria za usalama pamoja na kuhakikisha mabasi yao yamekaguliwa.
Samwix amesema madereva hawana sababu ya kukimbia kwani wanaharibu mfumo wa breki na kumaliza tairi za Mabasi na kusababisha hasara kwa wamiliki wa Mabasi
Mkurugenzi wa Sheria wa Mabalozi wa Usalama Barabani (RSA) Augustus Fungo amesema kuwa madereva wanawajibu wa kuwalinda abiria kwani ajali zinagharimu maisha.
Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA
Post a Comment