Katambi kutatua changamoto ya uzio Zahanati ya Old shinyanga | Tarimo Blog

Na Marco Maduhu, Shinyanga.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ameahidi kutatua changamoto ya ukosefu wa uzio katika Zahanati ya Oldshinyanga.

Katambi ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, amebainisha hayo leo kwenye mkutano wa hadhara Oldshinyanga.

Amesema amesikia kilio cha akina mama kwenye Kata hiyo, ambacho atakifanyia kazi, ili waendelee kupata huduma bora ya afya, pamoja na kuongeza watumishi na madawa, kwenye Zahanati hiyo.

"Katika Bajeti ya mwaka wa fedha (2021/2022) kuna Sh.biloni 45 ambazo zitajenga maboma nchi nzima, na bilioni 31,2 kujenga Zahanati 500, hivyo uzio wa kwenye Zahanati hii utajengwa tu mama zangu," amesema Katambi.

Katika hatua nyingine Katambi, ameahidi kutatua changamoto ya upungufu wa watumishi kwenye Zahanati hiyo ya Oldshinyanga, na ununuzi wa madawa.

Awali akiwasilisha kilio kwa niaba ya akina mama juu ya ukosefu wa uzio kwenye Zahanati ya Oldshinyanga, Diwani wa Vitimaalum Picca Chogelo, amesema wanawake wanaofika kujifungua wanapata shida wakati wa mazoezi, ambapo hukumbana na mifugo na kuhatarisha maisha yao.

Mbali na kuomba kujengewa uzio, pia wameomba kujengewa Jengo la mama na mtoto kwa ajili ya kujifungua, ambapo kwenye Zahanati hiyo halipo.

Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Patrobas Katambi, ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana na Ajira, akizungumza na wananchi wa Oldshinyanga kwenye mkutano wa hadhara.

Diwani wa Vitimaalum Picca Chogelo, akiwasilisha kero ya ukosefu wa uzio kwenye Zahanati ya Oldshinyanga na chumba cha kujifungua.


Wananchi wa Oldshinyanga wakiwa kwenye mkutano wa hadhara wa Mbunge Katambi.

Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

1/Post a Comment/Comments

Post a Comment

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2