RAIS DKT. HUSSEIN ALI MWINYI KUZINDUA TAMASHA LA 24 LA ZIFF2021 | Tarimo Blog

-Kushuhudia filamu ya Binti

Na Andrew Chale, Zanzibar.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye uzinduzi wa Tamasha la filamu za Nchi za  Majahazi (Zanzibar International Film Festival-ZIFF), kesho 21 Julai katika jukwaa la Ngome kongwe, Unguja, Zanzibar.

Akizungumza na Waandishi wa Habari, Mkurugenzi Mkuu wa ZIFF, Profesa Martin Mhando alisema tayari maandalizi yote yamekamilika kwa asilimia kubwa na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi amepata heshima ya kipekee kuwa mgeni rasmi.

"Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi atatuzindulia tamasha letu hili la 24 mwaka huu.
ZIFF pia tunaungana na Rais katika kuhakikisha uchumi wa bluu na ajira zikikuwa kwa vijana wetu kupitia filamu na shughuli zingine zitokanazo na uchumi wa bahari kama uvuvi wa bahari na Utalii." Alisema Prof. Mhando.

Katika tukio hilo la uzinduzi pia kutakuwa na burudani mbalimbali ikiwemo ya burudani kutoka kundi la Akeza Troup la Burundi, kikundi cha Kirua kutoa Zanzibar  na vingine vingi.

Katika hatua nyingine Prof. Mhando amebainisha kuwa wamejipanga kukabiriana na COVID 19 kwa kuzingatia kanuni zote za afya ambapo watakuwa na vifaa maalum vya kutakasa mikono pamoja na kuzingatia umbali wa mtu na mtu.

Katika tamasha hilo la ZIFF2021, Jumla ya filamu 65 zinatarajiwa kuoneshwa ikiwemo za Tanzania ni pamoja na; Binti, Decision, Dream, Murasi, Neema, Nyara, Salama, Shujaa wetu, Simba, Timela, Usiku mrefu, Nyundo, Kijiji changu huku  kwa Animation ama katuni ni Mbuland na Mozizi.

Filamu zingine ni pamoja na; A fool God, A trip of Heaven, Adam, Al sit, Carton rouge, Catch out, Coffee place, Days of Cannibalism, Deliveries, Bablinga, Bottleneck, Breaking ground, Dream child, Banyalga, Dreams of trains, Excuse, Fakh (The Trap), Heart attack, If Objects could talk na Interstate 8.

Pia zipo Itswa, Joy’s Garden, Letter to my child, Mission to rescue, Morning after, My culture my music, Naisula, Njaa, Nursery rhymes, Revolution, Shaina, Sikelela tapes, Softie, Sororal, Tales of the Accidental city, Tazara stories, The blind date, The Colonels stray, The fever, The Grandpa, The Handyaman, The Heartbeat, The Letter, To Zanzibar, Underestimated Villain, Walled Citizen na Why U hate.



Mafunzo ya Ufugaji Bora na Matibabu, Jiunge sasa kwa KUBOFYA HAPA

0/Post a Comment/Comments

Previous Post Next Post

Ad

Ads1

Sponsor Ad

Ads2